Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mtanzania aishiye Ujerumani aomba msaada kwa Rais Samia
Habari MchanganyikoTangulizi

Mtanzania aishiye Ujerumani aomba msaada kwa Rais Samia

Lucy Koble
Spread the love

MTANZANIA aishiye Ujerumani, Lucy Koble aliyeomba msaada kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezidi kuomba msaada kwa kiongozi huyo mkuu wa nchi kwani tangu alipotoa kilio chake mwaka jana hajapata msaada wowote kwake wala kwa mtoto wake. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka katika jiji la Munic nchini Ujerumani, Lucy alisema kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na ubalozi haujampatia msaada ili kutatua matatizo yake.

“Mimi pamoja na mtoto wangu tunaendelea kuteseka, tangu mwaka 2016 tumekuwa tukiwakilisha maombi yetu kwa ubalozi wetu huku Ujerumani, lakini hatujasaidiwa,” alisema.

Lucy ameeleza kuwa alienda nchini Ujerumani baada ya kuolewa na mwanaume raia wa nchi hiyo.

Aliongezea kuwa yeye na mwanae yamekuwa hatarini kabla na baada ya kujikuta akiwa chini ya utumwa utumiao wireless micro-sensors/implants, bila hiari na makubaliano yake kama ilivyo sheria huko aliko na sheria zote zihusikanazo na haki za binadamu duniani.

Alisema hivi karibuni, Lucy alimwandikia barua Rais akisema kuwa yeye pamoja na mtoto wake, wanahitaji msaada baada ya kuwekewa mwilini mwao bila ruhusa vifaa vinavyojulikana kama “wireless body Area micro- sensors/implants” ama “Theranostic sensor/implants”, ambavyo katika utaratibu wa afya hutumika kufanyia uchunguzi ili kutathmini tiba maalum za magonjwa na au kuendeleza tiba na uangalizi wa wagonjwa wenye magonjwa ya kudumu.

“Nimeshawasiliana na Waziri wetu wa Mambo ya Nje lakini naye amesema niwasiliane tu na Ubalozi wetu uliopo huku Ujerumani wao ndiyo watanisaidia, lakini sijasaidiwa,” alisema.

Alisema hivi karibuni, Lucy alimwandikia barua Rais akisema kuwa yeye pamoja na mtoto wake, wanahitaji msaada baada ya kuwekewa mwilini mwao bila ruhusa vifaa vinavyojulikana kama “wireless body Area micro- sensors/implants” ama “Theranostic sensor/implants”, ambavyo katika utaratibu wa afya hutumika kufanyia uchunguzi ili kutathmini tiba maalum za magonjwa na au kuendeleza tiba na uangalizi wa wagonjwa wenye magonjwa ya kudumu.

“Ila, sisi si wagonjwa. Ubadhirifu huu tulitendewa na watu ambao mpaka sasa hawajajulikana. Tumekuwa tukitumika kama wanyama wa maabara, tukiumizwa na kuteswa na hao wavunjao sheria ya haki zetu sisi kama binadamu,” alimweleza Rais katika Barua yake.

Aliongezea kuwa majaribio yanayofanyika yanahusisha maumivu makali mwilini na hali mbaya kiafya. Haki zao za uhuru wa kibinadamu zimepotea.

“Na si hizi tu zitakazoendelea kupotea bali pia, maisha yetu yako hatarini kupotea, kama serikali yetu haitatoa msaada au kuingilia kati.

“Ninakimbilia kwako Rais, kwa sababu juhudi zangu mwenyewe katika kutafuta msaada kwa muda mrefu sana hazijaleta matokeo yanayoweza kutusaidia,” alisema Lucy.

Baadhi ya vifaa hivi ni vya matoleo ya kisasa kabisa katika teknolojia ya jinsi hii ya kipekee, ambayo imefanya mkondo wa kisayansi unaouhusiana na sera na mifumo ya afya katika baadhi ya nchi zipate hatua mpya za kimaendeleo, hasa kwa sababau ya kuokoa muda wa mawasiliano baina ya madaktari na wagonjwa, na kuweza kukata matumizi makubwa ya kifedha.

Wao wamekuwa wakitumika kama wanyama wa majaribio ya kuendeleza matangazo, mauzo na kuboresha ubunifu katika sekta hii na nyinginezo zinazohusika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

Habari Mchanganyiko

Bodi ya Maji Wami Ruvu kuchimba visima 10 kupunguza uhaba maji mikoa mitatu

Spread the love  BODI ya Maji ya Bonde la Wami Ruvu imesema...

Habari za SiasaTangulizi

Bunge lalia msongamano wa mizigo bandari Dar es Salaam

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

Habari Mchanganyiko

NBC Dodoma International Marathon kutimua vumbi Julai 23

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetanganza msimu wa nne...

error: Content is protected !!