October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtanzania afungwa miaka 110 kwa ugaidi Kenya

Nyundo ya Hakimu

Spread the love

RAIA wa Tanzania, Abdul Harun Karim amefungwa miaka 110 jela nchini Kenya,  kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya kigaidi nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).  

Karim alihukumuiwa kifungo hicho na Mahakama ya Lamu mbele Hakimu Mkuu wa mahakama hiyo, T.A. Sitati tarehe 22 Mei 2019, baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka sita ya ugaidi yaliyokuwa yana mkabili nchini humo.

Miongoni mwa mashitaka yaliyo kuwa yana mkabili Karim ni pamoja, na kuwa gaidi wa kigeni, kuhamia nchini Somalia kwa lengo la kufundishwa masuala ya ugaidi na ukusanyaji wa taarifa kinyume na sheria ya kuzuia masuala ya ugaidi nchini Kenya.

Katika hukumu hiyo, ushahidi umethibitisha kwamba Karim alikutwa katika Kisiwa cha Kiwayu kilichopo Lamu  akiwa anajirekodi video iliyobeba ujumbe wa ‘bomu la kujitoa muhanga’ miaka mitatu iliyopita.

Aidha, katika shitaka lake lililokuwa lina mkabili la kuwa raia wa kigeni mwenye kujihusisha na masuala ya ugaidi Kenya, Karim alifungwa miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia.

Kwa mujibu wa mashitaka yaliyomtia hatiani Karim, mfungwa huyo alikamatwa mnamo tarehe 9 Mei 2019 kwenye kisiwa cha Kiwayu akiwa njiani kuelekea nchini Somalia kwa ajili ya kufundishwa masuala ya ugaidi. Ambapo mahakama hiyo ilimhukumu miaka 20 jela kwa kosa hilo.

Hakimu Sitati aliamuru Karimu kutumikia miaka 30 na 20 jela kwa wakati mmoja, kisha kutumikia kifungo cha miaka 60 jela kama adhabu ya makosa manne yaliyokuwa yana mkabili, ambapo kifungo hicho ni sawa na miaka 15 jela kwa kila kosa.

error: Content is protected !!