December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtangazaji Star TV, Radio Free Afrika afariki dunia

Spread the love

SAMADU Hassan aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha luninga cha Star Tv na Radio Free Africa, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe mosi Novemba 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Samadu amefikwa na umauti akiwa nyumbani kwake maeneo ya Miembe Mitatu wilayani Nyamagana jijini Mwanza, ambapo taarifa za awali zinaeleza kwamba alikuwa anasumbuliwa na kifua.

Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu Samadu, Latifa Hassan amesema hali ya kaka yake ilianza kubadilika ghafla ambapo walikwenda kutafuta usafiri kwa ajili ya kumpeleka hospitali, lakini isivyo bahati walivyorudi walikuta amefariki dunia.

Hata hivyo, Latifa amesema jana kaka yake alikuwa ana afya njema, na alikwenda kazini.

error: Content is protected !!