March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mtangazaji mpira azua kioja uwanjani

Spread the love

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Mtangazaji wa mpira nchini Urusi ameondoka uwanjani kabla mchezo haujaisha na kuwaacha watazamaji wakiangalia mechi hiyo bila maelezo.

Wakati wa mechi hiyo kati ya klabu ya Urusi ya Torpedo Vladmir dhidi ya Tekstilshchik Ivanovo kipa wa Ivanovo alimuangusha mshambuliaji wa upinzani kulingana na kanda za video.

Wakati wa tukio hilo timu hizo mbili zilikuwa 1-1. na baada ya kutolewa mkwaju wa penalti refa alitoa mkwaju wa adhabu nje ya eneo hatari na kusababisha malalamiko kutoka kwa mashabiki na watazamaji.

Na wakati mkwaju huo wa adhabu ulipopigwa mmoja ya walinzi waliunawa mpira na kuzua madai ya mkwaju mwingine wa penalti lakini refa aliwaambia wachezaji kuendelea na mchezo hatua iliyomlazimu mtangazaji huyo kumshutumu vikali refa huyo.

Hatua hiyo ilimkasirisha mtangazaji huyo na kuamua kusitisha matangazo aliyokuwa akitoa kulingana na ripoti za Pravda.

Na baada ya shutuma hizo ambapo mtangazaji huyo alimtajwa kwa jina la Nikolsky. “Aibu kubwa kwa soka ya Urusi, aliinuka na kuondoka huku akisema tazameni mechi bila mtangazaji leo.”

Mechi hiyo ilikamilika kwa timu zote mbili kufungana kwa bao 1-1.

error: Content is protected !!