May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtangazaji ITV auwawa

Marehemu, Blandina Sembu, Mtangazaji wa kipindi cha Jarida la Wanawake

Spread the love

 

BLANDINA Sembu, Mtangazaji wa kipindi cha Jarida la Wanawake kinachorushwa na kituo cha runinga cha ITV, ameuawa na watu wasiojulikana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumapili tarehe 28 Machi 2021, na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhan Kingai.

Kamanda Kingai amesema kuwa, mwili wa marehemu Sembu ulitupwa maeneo ya njia panda ya ITV, mbele ya Baa ya MaryLand, na watu wasiojulikana, waliokuwa wakitumia gari aina ya Toyota Noah.

Kamanda Kingai amesema baada ya mwili huo kuchunguzwa, ulikutwa na majeraha maeneo ya usoni.

Amesema Jeshi la Polisi mkoani humo lilipata taarifa kutoka kwa raia wema jana Jumamosi tarehe 27 Machi 2021, majira ya saa tano usiku.

“Tulichobaini katika uchunguzi wa awali marehemu hakuuliwa pale, mauwaji yalifanyika sehemu nyingine. Amekutwa na majeraha sehemu za usoni ambapo inaonekana alipigwa na kitu kizito usoni wakati anapambana kujitetea,” amesema Kamanda Kingai.

Kamanda Kingai amesema uchunguzi juu ya mauwaji hayo unaendelea kufanywa na Jeshi la Polisi Kinondoni.

error: Content is protected !!