Saturday , 2 December 2023
Home Kitengo Biashara Mtambo wa umeme Ubungo kupelekwa Mtwara
Biashara

Mtambo wa umeme Ubungo kupelekwa Mtwara

Spread the love

Imeelezwa kuwa, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) litapeleka mtambo wa umeme wa MW 20 mkoani Mtwara kutoka kituo cha umeme Ubungo  III ili kuimarisha hali ya umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara ikiwa ni utekelezaji wa agizo alilolitoa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko  la kuimarisha hali ya umeme katika mikoa hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Agizo hilo la kuimarisha hali ya umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara alilitoa wakati alipofanya ziara ya kikazi katika mikoa hiyo na kukuta hali isiyoridhisha ya upatikanaji umeme.

Hayo yamebainika wakati wa Kikao cha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko na Bodi pamoja na Menejimenti ya TANESCO kilichofanyika leo tarehe 21 Novemba 2023 jijini Dodoma.

Aidha, Dk. Biteko ameiagiza TANESCO kuongeza nguvu katika kutekeleza miradi ya uzalishaji umeme nchini kwa kutumia fedha zilizopo ili nchi iweze kuwa na umeme wa kutosha kusambazia wananchi ikiwemo umeme kutoka katika vyanzo vya nishati jadidifu.

Dk. Biteko pia ameitaka Bodi ya TANESCO kulisimamia vyema Shirika hilo na wafanye kazi kwa kushirikiana na Menejimenti kwani lengo la Shirika hilo ni kuhakiksha kunakuwa na umeme wa kutosha kwa matumizi mbalimbali.

Aidha, amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-hanga kusimamia na kuwatumia Watendaji na Wataalam wa shirika hilo vizuri ili kuwe na ufanisi katika shughuli zao za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme.

Dk. Biteko ameitaka TANESCO pia kuboresha Kitengo cha Huduma kwa Mteja kwa namna mbalimbali ikiwemo kuwaendeleza wataalam wanaotoa huduma kwa wananchi ili watoe huduma bora na yeye ameahidi kutoa ushirikiano kwa Shirika hilo pale utakapohitajika.

Dk. Biteko pia, ameitaka Bodi ya TANESCO kutokuwa na urasimu katika ufanyaji wa maamuzi na uzito wa kufuatilia masuala mbalimbali ili kutochelewesha miradi mbalimbali ya umeme.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba ameitaka Menejimenti ya TANESCO kuwa wabunifu na kuongeza nguvu katika ufuatiliaji wa vitu mbalimbali ikiwemo miradi na pia kuongeza umakini na kasi katika utendaji kazi  huku akieleza kuwa fedha za kutekeleza baadhi ya miradi hiyo zipo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Balozi, Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli amempongeza Dk. Biteko kwa kutoa miongozo mbalimbali ambayo inaendelea kuboresha utendaji kazi wa Shirika hilo na kueleza kuwa kikao hicho kimetoa njia ya wao kufanya kazi.

Aidha, ameahidi kutekeleza maagizo mbalimbali yaliyotolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, ikiwemo ya kuendeleza wataalam wanaofanya kazi katika Kitengo cha Huduma kwa Mteja.

Katika kikao hicho TANESCO imeeleza hatua mbalimbali wanazochukua ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme kwenye baadhi ya mikoa ikiwemo Dar es salaam hasa katika maeneo ya Temeke na Kinondoni ambako kuna ongezeko la mahitaji ya umeme.

Imesema tayari hatua mbalimbali zitachukuliwa ikiwemo kuongeza uwezo wa miundombinu ya kusafirisha umeme kwa kujenga njia za kusafirisha umeme kutoka Kinyerezi hadi Mbagala kupitia Gongo la Mboto kwa ajili ya Wilaya ya Temeke hadi Mkuranga.

Njia nyingine inayojengwa ni ya kusafirisha umeme kutoka Ubungo hadi Ununio ili kuimarisha upatikanaji umeme maeneo ya Mbezi Beach, Kunduchi na Mikocheni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Shinda mtonyo mrefu ukicheza Shaolin Crew kasino ya  Meridianbet

Spread the love  TAIFA la Uchina limebebwa na historia kubwa sana, wengi...

Biashara

Kasino ya Lucky Sevens ni rahisi kucheza na kuibuka tajiri, fanya haya

Spread the love  NENO Kasino unapolisikia kwa mara ya kwanza unapata picha...

Biashara

Ujenzi waiva barabara ya Bigwa – Kisaki

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa mkandarasi atakayetekeleza ujenzi...

Biashara

Fanya haya kabla hujacheza kasino

Spread the love  UNAPOANZA kufikiria jinsi ya kutengeneza pesa kirahisi usipate shida,...

error: Content is protected !!