July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtaka apiga ‘Stop’ daladala kusimamisha abiria, kisa Covid-19

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (RC), Anthony Mtaka

Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, amepiga marufuku mabasi ya abiria ‘daladala’, kusimamisha abiria, ili kudhibiti maambukizi ya mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (Covid-19). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Mtaka ametoa agizo hilo leo Jumamosi, tarehe 10 Julai 2021, katika ziara ya Waziri wa Afya, Dk. Dorothy Gwajima, kwenye Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Mkuu wa mkoa huyo, ameagiza madereva wabebe abiria kulingana na idadi ya siti za magari hayo, kwa ajili ya kukwepa mikusanyiko ya watu.

“Jukumu la Serikali limeshaisha kwa kuwatangazia wananchi kujikinga, kwa maana ugonjwa wa Corona upo na wagonjwa wameanza kuonekana nchini,” amesema Mtaka.

Mtaka ameongeza “na sisi kama mkoa tumedhamiria kuanza na maeneo ya stendi, kwa kila gari kuacha kusimamisha abiria ndani ya gari na hili tunaomba wafanya biashara wa magari watuelewe.”

Wakati huo huo, Mtaka amewataka wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali katika mkoa huo, wachukue tahadhari za kujikinga na Covid-19, ikiwemo kuvaa barakoa na kunawa mikono mara kwa mara.

Naye Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Devis Mwamfupe, amesema Covid-19 ni janga la dunia, hivyo wananchi hawapaswi kusubiri maelekezo ya Serikali ili waanze kujilinda.

“Nipende kusema suala la ugonjwa wa Covid -19 awamu ya tatu, ni ugonjwa unaolikumba Taifa. Kutokana na hali hiyo, ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha analinda afya yake bila kusubiri maelekezo kutoka ngazi ya Taifa” amesema Mwamfupe.

error: Content is protected !!