Saturday , 15 June 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Mtaka akaidi agizo la Prof. Ndalichako hadharani
ElimuTangulizi

Mtaka akaidi agizo la Prof. Ndalichako hadharani

Prof. Joyce Ndalichako
Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, amekaidi kutii agizo la Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, la kuzuia masomo ya ziada, kwa wanafunzi walio katika maandalizi ya mitihani ya kitaifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Prof. Ndalichako alikazia agizo hilo katika mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2021/22, uliofanyika Juni 2021, bungeni jijini Dodoma, kwa maelezo kwamba utaratibu huo unakwenda kinyume na sera ya elimu bila malipo, kwa kuwa wananchi wanachangishwa fedha.

Akizungumza na baadhi ya wazazi na walezi wa wanafunzi wa kidato cha nne mkoani humo, leo tarehe 13 Julai 2021, Mtaka amesema katika suala la elimu, hatofuata ushauri wa watu aliowaita wanasiasa.

“Suala la elimu kwangu ni kipaumbele na sitahitaji ushauri wa wanasiasa kwenye jambo hili,” amesema Mtaka.

Mtaka amewataka wakuu wa wilaya na mameya wa halmashauri za mkoa huo, wawaruhusu wanafunzi walio katika madarasa ya kufanya mitihani ya kitaifa, hasa kidato cha nne, kuweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na mitihani hiyo.

“Mkuu wa wilaya, meya na wenyeviti, shule za Dodoma watoto walio form four (kidato cha nne) waruhusuni wafanye kambi za kitaaluma ili wajiandae na mitihani. Akifaulu ndiye atakayekutoa kwenye kina cha maji mengi, mimi nimekutana na ninyi wazazi na nitakutana na walimu,” amesema Mtaka.

Bila ya kumtaja jina, Mtaka amedai kuwa, anayekataza wanafunzi wasisome masomo ya ziada hasa wa shule za kata za Serikali, watoto wake wanasoma katika shule nzuri binafsi ambazo hazina uhaba wa walimu.

“Hao wanaowaambia watoto wao wanasoma shule za ada ya Sh. 10 milioni, hawaosmi shule za kata. Yaani maana yangu ni kwamba, usisikilize ushauri wa waziri anayekwambia kusiwe na kambi. Muulize waziri kwani watoto wako mwenzetu wanasoma wapi? Mwenzako mtoto anasoma Canada hajui kama hakuna mwalimu wa fizikia wala kemia,” amesema Mtaka.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (RC), Anthony Mtaka

Mtaka ameongeza “ yeye amekaa kwenye kiyoyozi anakwambia watoto kusoma mwisho saa tisa mchana, kama watoto wanasoma mpaka saa 11 jioni maana yake shule na walimu wamekubaliana wawasaidie watoto kwenye masomo ya ziada kwa ajili maandalizi.”

Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma amedai kuwa, watoto wa wanasiasa wengi husoma masomo ya ziada na katika shule nzuri za watu binafsi, ndiyo maana hawafanyi vibaya katika matokeo yao ya mitihani ya kitaifa.

“Akitoka kwenye televisheni anakuambia mwisho watoto kusoma saa tisa, anasubiri atangaze watoto wako wamepata sifuri na division four kwenye matokeo, msikilizeni mkuu wa mkoa anayewaambia watoto waende kambi wafanye maandalizi,” amesema Mtaka.

Katazo la wanafunzi kusoma masomo ya ziada, lilipingwa na baadhi ya wabunge katika mjadala wa bajeti, uliofanyika mwishoni mwa Juni 2021.

Mbunge wa Bukoba Vijijini mkoani Kagera (CCM), Jason Rweikiza, ni miongoni mwa wabunge waliopinga katazo hilo, akisema kwamba linalenga kudumaza maendeleo ya wanafunzi.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma, tarehe 21 Juni mwaka huu, Rweikiza alisema wanafunzi wengi wanaofeli mitihani yao, hushindwa kurudia tena mtihani kutokana na gharama, hali inayosababisha ndoto zao za elimu kuishia hapo.

2 Comments

  • Waachiwe wazazi pia wachangie kitu kidogo kwa waalimu wa masomo ya ziada kwani pia ni motisha kwa wazazi kufanya kazi kwa bidii na kuweka akiba ya kipato chao ilikuja kulipia “tuition” hizi. Ni njia pia ya kuongeza pato la taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

Habari za SiasaTangulizi

Bilioni 155.4 kugharamia kicheko cha wastaafu 2022-2030

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh...

BiasharaHabari za SiasaTangulizi

Ushuru kwenye bia, urembo kuchangia bima ya afya

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

error: Content is protected !!