Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Mtaalam wa uchumi’ Z’bar achukua fomu ya urais CCM
Habari za Siasa

‘Mtaalam wa uchumi’ Z’bar achukua fomu ya urais CCM

Omary Sheha Mussa, Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Spread the love

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anayejitambulisha kuwa mtaalamu wa uchumu, Omary Sheha Mussa amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais wa Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Mussa amechukua fomu hiyo leo Jumatano tarehe 17 Juni 2020 visiwani Zanzibar, ambapo alikabidhiwa na Galos Nyibo, Katibu wa Oganaizesheni CCM Zanzibar

Mussa amesema, endapo atapata ridhaa ya CCM kugombea urais na kisha kuchaguliwa na Wazanzibar, atakuwa kimbilio na msaada kwa wananchi wanyonge hasa wanaopokonywa mali zao.

“Mimi kwa sasa siko serikalini, niko nje ya serikali na mara nyingi ukiwa nje unaona makosa ndani ya serikali, huwezi kusema ukiwa nje lakini ukipata nafasi unasawazisha. Nimeona wapo wananchi wanalalamika ardhi zao zimepokonywa, pesa zao zimechukuliwa,” amesema Mussa na kuongeza:

“Sasa hayo yapo, lakini katika hali hiyo hao wenzetu wamejitahidi na mimi nasema, nitajitahidi mazuri yao nitayaendeleza, na ndio MwanaCCM anatakiwa awe hivyo, aendeleze yale mazuri aliyoanza mwenzake.”

Mussa amesema, endapo atapata ridhaa ya CCM kugombea urais, kisha kushinda nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020, atabadilisha mfumo wa Serikali ya Zanzibar, ili kuimarisha uchumi na kuleta maendeleo ya Zanzibar na wananchi wake kwa ujumla.

Amesema, endapo atafanikiwa kuwa Rais wa SMZ, ataweka sera rafiki zitakazowezesha ukuaji wa sekta ya utalii.

“Nakusudia kubadilisha mfumo wa Zanzibar, kufanya mambo yafuatayo; kuongeza pato la taifa kutoka lilipo hadi liende mbele. Mimi kazi yangu ni kutafuta fedha na hakika nalo naliweza.

“Nina mpango wa kuongeza mapato ya utalii, Zanzibar inategemea sana mapato ya utalii, uchumi wa Zanzibar ni huduma lakini kati ya hiyo asilimia 20 ni utalii,” amesema Mussa.

Mussa anakuwa kada wa tatu wa CCM kuchukua fomu, baada ya Mbwana Bakari Juma kufungua dimba hilo Jumatatu ya tarehe 15 Juni 2020, akifuatiwa na Ally Abeid Aman Karume, mtoto wa Sheikh Abeid Karume, aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Spread the loveWATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

error: Content is protected !!