September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Msuva atoa siri ushindi Stars

Spread the love

KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Simon Msuva ametoa siri yabushindi kwenye mchezo wa kimataifa wa kufuzu fainali za kombe la Dunia dhidi ya Madagascar. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa kundi J, uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, ulimalizika kwa Taifa Stars kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Mara baada ya mchezo huo, nyota huyo ambaye anakipiga kwenye klabu ya Wydady Casablanca alisaema kuwa wakati wa mapumziko timu hizo zikiwa zimetoka sare ya mabao 2-2, kocha mkuu wa kikosi hiko Kim Poulsen aliwaambia wahahakikishe ndani ya dakika 10 za kwanza kwenye kipindi cha pili wanapata bao.

“Baada ya kwenda mapumziko kocha alituambia tujipange, ndani ya dakika 10 tuwe tumepata bao, sisi tukamsikiliza mwalimu na tukaweza kupata bao ndani ya dakika 10” Alisema Msuva

Katika mchezo huo Stars ilitangulia kupata mabao mawili kupitia kwa Erasto Nyoni, aliyefunga kwa njia ya penati kwenye dakika ya 3, na kisha baadae Novatus Dismas akaandika bao la pili kwenye dakika ya 27.

Kabla ya kwenda mapumziko kikosi cha Madagascar kilichomoa bao hizo kupitia kwa Thomas Fountain na kufanya timu hizo kwenda mapumziko huku zikiwa zimefungana mabao 2-2.

Kipindi cha pili kiliporejea kiliwachukua Stars dakika nane kuandika bao la tatu kupitia kwa Feisal Salum na kufanya mchezo huo kutamatika kwa Stars kutoka kifua mbele.

Kwa matokeo hayo, Stars inapanda mpaka kwenye kilelel cha msimamo wa kundi J, ikiwa na pointi nne, sawa na Benini.

error: Content is protected !!