June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msuva ang’ara Tuzo za Vodacom

Baba mzazi wa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akipokea zawadi ya mfungaji bora kwa niaba ya mwanaye

Spread the love

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Simon Msuva ameng’ara kwenye tuzo za wadhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom, baada ya kutwaa tuzo mbili.

Msuva amebeba tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu akiwashinda beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba SC na Mrisho Ngassa waliyekuwa naye Yanga SC kabla ya kutimkia Afrika Kusini.

Msuva ambaye hakuwepo ukumbini kutokana na kuwa katyika kikosi cha timu ya Taifa kilicho kambini Ethiopia kikijiandaa na mchezo wao na Misri, aliwakilishwa na baba yake mzazi, kuchukua tuzo mbili za mfungaji bora wa msimu wa 2014/15 na tuzo ya mchezaji bora wa msimu.

Mshambuliaji huyo alifanikiwa kutwaa tuzo ya mfingaji bora baada ya kufunga mabao 17 katika msimu huo, huku akiisaidia timu yake ya Yanga kutwaa ubingwa wa msimu huo, hivyo kuzawadiwa tuzo ya mchezaji bora wa msimu, pamoja na tuzo lakini ametwaa kitita cha jumla ya Sh. 11.4 milioni, yaani Sh. Sh. 5.7 milioni kwa kila tuzo aliyotwaa usiku wa leo.

Tuzo ya Kiatu cha dhahabu alichozawadiwa Simon Msuva
Tuzo ya Kiatu cha dhahabu alichozawadiwa Simon Msuva

Katika hafla hiyo Yanga walizawadiwa zawadi yao ya ubingwa ambayo ni mfano wa hundi ya Sh. 80.4 milioni kutoka kwa wadhamini hao, hukuAzam FC Sh. 40.2 milioni kwa kuwa wa pili, Simba Sh 28.7 milioni kwa kuwa wa tatu na Mbeya City Sh. 22.9 milioni kwa kuwa nne.

Tuzo nyingine zilizotolewa katika sherehe hizo ilikuwa ni ya kipa bora ambayo imekwenda kwa aliyekuwa kipa wa Coastal Union, Shaaban Kado ambaye amezawadiwa kitita cha Sh. 5 milioni.

Mbwana Makatta amewashinda Mserbia Goran Kopunovic aliyekuwa Simba SC na Mholanzi Hans Van Der Pluijm wa Yanga SC katika tuzo ya kocha bora, baada ya kuinusuru Prisons kushuka daraja na kuzawadiwa Sh. 8.6 milioni.

Israel Nkongo amewashinda Jonesia Rukyaa na Samuel Mpenzu katika tuzo ya Mwamuzi Bora na kupata Sh. Milioni 8.6, wakati Mtibwa Sugar imezipiga kumbo  Mgambo JKT na Simba SC katika tuzo ya timu yenye Nidhamu na kuzawadiwa Sh. Milioni 17.2.

Mgeni Rasmi katika hafla hizo alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Juma Nkamia. Zawadi zinazotolewa msimu zina thamani ya Sh 232 milioni.

error: Content is protected !!