Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Msukuma awatisha Usalama wa Taifa
Habari za SiasaTangulizi

Msukuma awatisha Usalama wa Taifa

Joseph Kasheku "Msukuma" Mbunge waa Jimbo Geita Vijijini na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Geita
Spread the love

JOSEPH Kasheku “Msukuma” Mbunge waa Jimbo Geita Vijijini na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Geita ametoa siku tano za kuombwa na radhi na wanaodaiwa kuwa ni maofisa usalama wa Taifa waliotoa taarifa za uongo dhidi yake na kusababisha akamatwe Mjini Dodoma, anaandika Charles William.

Juzi Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, liliwatia nguvuni Msukuma, Hussein Bashe, Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini na Adam Malima, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga kwa madai ya kupanga kufanya vurugu katika Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika jana.

Wanasiasa hao walikamatwa na kuhojiwa, kabla ya kuachiwa kwa dhamana. Hata hivyo Msukuma amesema hawezi kukaa kimya juu ya suala hilo na kwamba wapo maofisa usalama waliosambaza taarifa juu yake na kusababisha hofu lazima wamuombe radhi.

“Hawa ni wapiga dili, Rais lazima aiangalie upya Idara ya Usalama wa Taifa. Wameniundia mimi zengwe, mpaka nikakamatwa, na nchi ikawa kwenye presha, kama chama kisipozungumza mimi nitaenda kuzungumza na watoto wangu kama Askofu Gwajima (Josephat),” amesema.

Mbunge huyo anayesifika kwa vituko visivyoisha, amesema atapigania heshima yake kwani hajawahi kupata kashfa na lazima atashinda.

“Sitazungumza kitaifa, nitaenda kuzungumza na wapiga kura jimboni kwangu, nieleze kwanini watu wametengeneza kinyago wakakiweka sebuleni halafu kinawatisha wenyewe. Kama kuna usalama wa taifa aliyeshiriki natpa siku tano awe ameniomba msamaha,” amesema Msukuma.

Hofu ya kuibuka kwa vurugu katika mkutano mkuu wa CCM uliofanyika jana iliibuka baada ya juzi Halmashauri Kuu – NEC ya chama hicho kuchukua uamuzi wa kuwafukuza viongozi mbalimbali wanaodaiwa kuwa walikisaliti chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Waliofukuzwa uanachama ni pamoja na wenyeviti wa CCM katika mikoa minne wakiwemo Ramadhani Madabida (Dar es Salaam) na Jesca Msambatavangu (Iringa). Sophia Simba, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum alikutana na kadhia hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!