May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msukuma amtuhumu RC Geita, wenzake kujilipa posho milioni 600

Joseph Kasheku 'Msukuma,' Mbunge wa Geita Vijijini

Spread the love

 

MBUNGE wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma amesema, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel na timu yake wamejilipa Sh.600 milioni, fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii (CSR). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Msukuma amesema hayo leo Alhamisi, tarehe 29 Aprili 2021, bungeni jijini wakati akichangia bajeti ya wizara ya madini kwa mwaka 2021/22, iliyowasilishwa na waziri wake, Doto Biteko.

Katika mchango wake, Msukuma amekosoa utaratibu wa fedha za CSR zinazotolewa, kuwa zinagawanya na mkuu wa mkoa mwenyewe badala ya jukumu hilo, kufanywa na halmashauri husika za Geita na Geita Vijijini.

Amesema, halmashauri hizo, zinapata Sh.10 bilioni za CSR zinazotolewa na mgodi wa madini wa GGM, “lakini haina mpangilioni, kama nilikitu tu limetupwa halina mwenyewe. Wizara ya madini na Tamisemi, ni nini kiliwafanya mkamwachia mkuu wa mkoa awe anatuamilia sisi?”

“Yaani mkuu wa mkoa amepewa mamlaka ya kutuamlia sisi, kajenge darasa, kajenge hoteli, kuna vitu vingine vinauma.”

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel

Msukuma amesema, “mimi nina nyaraka hapa, kwa mwaka mmoja halmashauri ya Geita na Geita mjini, mkuu wa mkoa na timu yake wamejilipa posho milioni 600, hii haiwezekani.”

Mbunge huyo amemtaka Waziri Biteko, kulitolea ufafanuzi suala hilo.

error: Content is protected !!