Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Msongamano wanafunzi darasani wazitesa shule Tunduma
Elimu

Msongamano wanafunzi darasani wazitesa shule Tunduma

Spread the love

 

WANANCHI katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe wameiomba serikali kuongeza vyumba vya madarasa katika shule za msingi ili kuondokana na msongamano wa wanafunzi uliopo. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea).

Maimuna Mtafya, mkazi wa Sogea akizungumza na MwanaHALISI Online amesema baadhi ya shule zilizopo katika mji huo zimekuwa na mrundikano mkubwa wa wanafunzi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.

Amesema hali inayowapa wakati mgumu walimu kufundisha na hata wanafunzi kushindwa kuelewa vizuri masomo hali inayoweza kufifisha ufaulu.

Grace Mwakajila, mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Sogea, amesema licha ya serikali kujenga shule nyingine ya ghorofa pembezoni mwa shule hiyo, lakini bado msongamano upo.

Amesema awali walikuwa wanakaa wanafunzi 150 darasa moja lakini baada ya ujenzi wa shule hiyo ya Haisoja wanakaa 100 idadi ambayo ni kubwa kuliko inavyoelekezwa kwenye Sera ya Elimu.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Sogea, Charles Kwilasa, amesema Serikali imefanya kazi yake kujenga shule hizo za ghorofa kupunguza msongamano.

“Kazi yetu sasa ni kuhamasisha wazazi kuwapeleka watoto shule sambamba na kuhamasisha utoaji wa vyakula ili watoto wapate angalau mlo mmoja akiwa shuleni ili waweze kufanya vyema kwenye masomo,” amesema Kwilasa.

Mkuu wa shule ya msingi Sogea, Hamad Mwangomale, amesema serikali imefanya jambo zuri kujenga shule pacha iitwayo Haisoja ya ghorofa ikiwa na vyumba 10 vya madarasa hali iliyopunguza kwa kiasi msongamano.

“Lakini bado, kabla ya ujenzi wa shule hiyo watoto walikuwa wanakaa 150 baada ya ujenzi wanakaa 100 katika chumba kimoja cha darasa badala ya 45 iliyopo kisheria,” amesema.

“Shule ya Haisoja ina wanafunzi 999 kuanzia darasa la awali hadi la nne, shule mama ya Sogea wamebaki na wanafunzi 2,530 idadi ambayo bado ni kubwa.”

Aidha amesema hali ya utoro kuwa ni asilimia 30 na kuwataka wazazi kuwafutilia mienendo ya watoto wao badala ya kuwaachia walimu pekee.

Pia ameiomba Serikali kuwaongezea walimu 43, nyumba za walimu, maji, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, matundu 77 ya vyoo vya wanafunzi, matundu mawili ya vyoo vya walimu na vyumba 41 vya madarasa.

Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri hiyo,Katherin Mbawala amesema uwepo wa maeneo madogo, na muingiliano wa watu wanaofika kufanya biashara kwenye mpaka huo imesababisha ongezeko kubwa la watoto na kuzifanya shule kuelemewa.

Hata hivyo amesema tayari uongozi wa halmashauri, madiwani, watendaji wamefanya vikao kutafuta utatuzi wa changamoto hizo.

Amesema baada ya wazo kupitishwa kwenye vikao Mkurugenzi mtendaji alibariki ujenzi wa shule ya Haisoja ya ghorofa kwa Sh 800 milioni fedha za mapato ya ndani na kujenga shule nyingine ya Kokoto kwa gharama kama hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji Tunduma Philimon Magesa, amesema kutokana na ufinyu wa maeneo wameamua kujenga shule za ghorofa.

“Kimsingi eneo la shule linatakiwa kuwa hekari tatu au zaidi na sasa shule hizo mbili zipo asilimia 98 na sasa wanajipanga kujenga jengo lingine la ghorofa pacha kuondoa kabisa msongamano,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

error: Content is protected !!