Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Msomi IFM adakwa akitaka kukodisha Bastola
Habari Mchanganyiko

Msomi IFM adakwa akitaka kukodisha Bastola

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imemtia mbaroni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Robson Maji (21)kwa kosa la kukutwa akitaka kuuza bunduki aina ya Bastola yenye risasi, anaandika Faki Sosi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa mwanafunzi huyo alikamatwa akiwa kwenye mipango ya kuuza Bastola aina ya Beretta yenye namba DAA316502 ikiwa na risasi sita.

Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo lilipata taarifa ya kuwepo kwa biashara ya kukodishwa kwa silaha kwa majambazi ili wakafanyie kazi za kiuhalifu na kulipwa fedha na kwamba uliandaliwa mtego maeneo ya TRA Mwenge na kumkamata mtuhumiwa akitaka kukodisha kwa Sh.. 400,000.

Mtuhumiwa huyo aligunduliwa kuwa yupo tayari kuiuza kwa Sh. 2,500,000 na kwamba alipohojiwa alikiri kuiba silaha hiyo kwa Baba yake aitwaye Isaack Maji (51) mkazi wa Tabata Segerea.

Mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alitaja mshirika wake ambaye ni rafiki yake mwanafunzi wa Chuo cha Columbus Staste Cummunity cha nchini Marekani.

Amesema upelelezi unaendelea ili kujua mmiliki halali wa silaha hiyo na mahojiano zaidi yanafanyika ili kuweza kubaini silaha hiyo imekodishwa mara ngapi na imetumika na watu gani

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!