Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msiri wa Prof. Lipumba ajiuzulu, sababu ‘zazimwa’
Habari za Siasa

Msiri wa Prof. Lipumba ajiuzulu, sababu ‘zazimwa’

Spread the love

MTU wa karibu na msiri wa Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Abdul Kambaya amejiuzulu nafasi ya ukurugenzi wa Idara ya Habari, Uenezi na mahusiano ya Umma ya chama hicho. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zimeeleza, Kambaya ameandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo ambapo, Prof. Lipumba ameridhia uamuzi huo. Hata hivyo, CUF haijaeleza sababu za kujiuzulu kwake.

“Ni kweli lipo jambo zito lililomsukuma, lakini kwa sasa siwezi kukwambia,” amesema ofisa mmoja wa CUF aliyeulizwa sababu za kujiuzulu Kambaya.

Taarifa za awali zinadai, Kambaya anatuhumiwa kushindwa kutosha katika nafasi hiyo na kwamba, CUF imekuwa haipati nafasi kwenye vyombo vya habari.

Mtandao huu umemtafuta Kambaya ili kujua ukweli wa tuhuma hizo, hata hivyo amesema anayepaswa kueleza sababu za kujiuzulu ni Prof. Lipumba.

“Prof. Lipumba ndio aeleza sababu za mimi kujiuzulu. Barua niliyomuandikia ina sababu zote, muulizeni yeye,” amesema Kambaya na kuongeza;

“Haiwezekani mtu kusema, mtu amejiuzulu halafu asitoe sababu za mhusika kujiuzulu, bila shaka huyo aliyetoa taarifa ya kujiuzulu alipaswa akamilishe taarifa kwa kueleza sababu za kujiuzulu, sipaswi mimi tena kuwa mtoa taarifa hapana.”

Mtandao huu ulimtafuta Prof. Lipumba ili kujua zaidi kuhusu sababu za Kambaya kujiuzulu, hata hivyo simu yake iliita bila kupokewa.

Alipotafutwa Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara na mbunge wa Kaliua mkoani Tabora ameeleza, tuhuma kwamba ameshindwa kwenye nafasi hiyo hazina ukweli, pia ameshindwa kueleza sababu za kujiuzulu Kambaya.

“Sababu zake sizijui, sababu najua mwenye mamlaka ya kuteua ni mwneyekiti, Katiba imempa mamlaka ya kuteua na kutengua.

“Kambaya alivyojisikia kujiuzulu, akapeleka barua kwa aliyemteua, kwa kuwa alipeleka barua kwa mwenyekiti aliyemteua, yeye ndiye atakayejua sababu,” amesema Sakaya.

Kambaya ni miongoni mwa watu wa karibu wa Prof. Lipumba, mbapo mara kadhaa amekuwa akimuhusisha kwenye uamuzi wake.

Nafasi ya Kambaya imechukuliwa na Mohamed Ngulangwa. Uteuzi mwingine uliofanywa leo tarehe 23 Januari 2020, ni kuwa Mnake Jafar ameteuliwa kushika nafasi ya Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Bunge na Sera na Juma Kilaghai ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi.

Kwa mujibu wa barua ya CUF, mabadiliko hayo yatakamilika baada ya kuthibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi CUF Taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!