August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msigwa ataka Ikulu iuzwe

Spread the love

Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa mjini (Chadema) amemshauri Dk John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuuza kwanza Ikulu kabla ya kuuza majengo mengine ya serikali ili zipatikane hela za kuhamia Dodoma, anaandika Josephat Isango.

Msigwa amesema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook na kusisitiza kuwa haamini kama watanzania ni kama ng’ombe wataswagwa swagwa tu.

“We have a serious challenge as a National(tunachangamoto hasa kama taifa), nimshauri Rais aanze kwanza kuuza Ikulu ndipo majengo mengine ya umaa yafuate, nadhani ikulu itapata wateja mapema , tutapata hela za kuhamia Dodoma.” Ilisomeka kauli ya Msigwa.

Mbunge huyo pia amesema haamini kuwa watanzania nikama ng’ombe ambao wataswagwa swagwa tu wakae kimya, na kuonya kuwa mengi watayaona ambayo bado hayajajiri.

Kauli ya Msigwa inakuja ikiwa ni wiki tu tangu serikali ya Magufuli kutangaza mpango wake wa kuhamishia serikali yote mkoani Dodoma kabla ya mwaka 2020.

Magufuli alitoa kauli hiyo, wakati akihutubia mkutano mkuu maalum wa chama chake – Chama  Cha Mapinduzi (CCM) – tarehe 23 Julai. Mkutano mkuu wa CCM uliomalizika mkoani Dodoma wiki iliyopita, ulimchagua Dk. Magufuli, kuwa mwenyekiti wa tano wa chama hicho.

Katika hotuba yake mbele ya wajumbe, Magufuli ameeleza kile alichoita, “dhamira yake ya dhati ya kukamilisha mpango wa serikali wa kuhamia Dodoma.”

Uamuzi wa kuhamishia makao makuu ya serikali mkoani Dodoma, umeonekana kupokelewa kwa hisia tofauti tangu ulipotangazwa wengi wakisema uamuzi huo unafanyika kwa papara na bila maandalizi.

Katika bajeti ya serikali iliyopitishwa na Bunge mwezi uliyopita, hakukutengwa fedha zozote kwa ajili ya kazi hiyo.

 

error: Content is protected !!