August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msiba CUF kuwakutanisha Maalim, Lipumba

Spread the love

ASHURA Mustafa, aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF) amefariki dunia leo asubuhi, anaandika Faki Sosi.

Mjumbe huyo amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako imeelezwa alikuwa akisumbuliwa na upungufu wa damu na kwamba, taratibu za mazishi yake bado zinafanywa.

Kwenye msiba huo, Prof. Ibrahim Lipumba, aliyekuwa katika Mikoa ya Kusini, anatarajiwa kuhudhuria.

Prof. Lipumba leo asubuhi amesitisha ziara yake kwenye Wilaya ya Newala, Mtwara ili kurejea jijini Dar es Salaam kushiriki mazishi ya Ashura katika wakati utakaopangwa na familia yake.

Pia msiba huo pia unatarajiwa kuhudhuriwa na Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa chama hicho.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa Ashura zinaeleza kuwa, mjumbe huyo aliyesimamishwa uanachama na chama chake katika mgogoro wa ndani wa chama hicho unaoendelea kwa sasa, alilazwa takribani wiki moja iliyopita Muhimbili.

Taarifa zaidi zitawajia….

error: Content is protected !!