MTU anayetuhumiwa kumuua Waziri Mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa hali yake ya kiakili ili kutathmini afya yake ya kiakili wakati wa tukio hilo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Abe aliuawa kwa kupigwa risasi kwenye kampeni tarehe 8 Julai, 2022 katika mji wa magharibi wa Nara, siku mbili kabla ya uchaguzi wa bunge nchini humo.
Mshukiwa wa muuaji hayo Tetsuya Yamagami mwenye umri wa miaka 41 yuko kizuizini na inasemekana alimlenga Abe kwa kuwa aliamini kiongozi huyo wa zamani alihusishwa na Kanisa la Muungano.
Mahakama ya Wilaya ya Nara iliidhinisha ombi la ofisi ya waendesha mashitaka la kufanyika uchunguzi wa kiakili unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.
Abe alikuwa mwanasiasa mashuhuri na maarufu zaidi nchini Japan, alijiuzulu mwaka 2020 kutokana na sababu za kiafya.
Leave a comment