August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mshtuko wa ugaidi, 11 wanaswa

Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Mwanza, linawashikilia watu 15 wakiwemo watoto 11 wenye umri wa miaka 10 wakidaiwa kufundishwa ‘ugaidi’ katika nyumba moja iliopo Kishiri nje kidogo ya jiji hilo, anaandika Moses Mseti.

Kabla ya kufika kwenye nyumba waliyokuwemo watuhumiwa, polisi walimkamata kijana mmoja kwenye Kata ya Kishiri, Wilaya ya Nyamagana ambaye alidaiwa kuhusika.

Baada ya kumkamata kijana huyo (jina linahifadhiwa), walimtaka awapeleke mahali ambapo ‘mafunzo’ hayo yanafanyika jambo ambalo lilitekelezwa.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi, Ahmed Msangi amethibitisha kukamatwa kwa watu hao na kueleza kuwa, walifanikiwa kuwakamata baada ya taarifa kutoka kwa kijana huyo.

Msangi ameeleza kuwa, baada ya taarifa za kijana huyo ambaye aliyeongozana na polisi hadi katika eneo la tukio, waliwakuta watuhumiwa hao.

Amesema, watuhumiwa hao baada ya kugundua kuwa ni polisi, walirusha bomu moja jambo ambalo liliwasukuma polisi kuanza kujibu mashambulizi kwa  kupiga risasi hewani na kuwamuru kujisalimisha.

Kamanda Msangi amedai kuwa, baada ya watu hao kujisalimisha, polisi walianza kufanya ukaguzi katika nyumba hiyo na kufanikiwa kukuta bunduki aina ya SMG na magazine tano zilizokuwa na risasi 150.

Ameeleza kuwa, polisi pia walifanikiwa kukamata vitabu viwili vya Dini ya Kiislamu na kofia moja ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi  wa Tanzania (JWTZ).

Na kwamba, kitendo hicho amedai kinashabiana na vitendo vya ugaidi na matukio mengine yaliowahi kufanyika jijini humo.

“Kama mtakuwa mnakumbuka vizuri kuna matukio ambayo yalishawahi kutokea hapa Mwanza yakiwemo ya msikitini watu kuchinjwa, na watu wanaodai inaweza ikawa ndio hao wahusika,” amesema Msangi.

error: Content is protected !!