Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mshtuko! Mdude wa Chadema apatikana akiwa hoi
Habari za SiasaTangulizi

Mshtuko! Mdude wa Chadema apatikana akiwa hoi

Spread the love

MWANAHARAKATI na Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mdude Nyagali amepatikana akiwa hoi baada ya kutupwa kwenye Kijiji cha Mkwenje, Kata ya Inyala jijini Mbeya. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa za kupatikana kwa Mdude zilianza kutolewa jana tarehe 8 Mei 2019 na Diwani wa Kata ya Nsalala, Kisman Mwangomale ambaye  amesema, alipigiwa simu na wakazi wa Makwenje na kumwomba msaada wa haraka wa kwenda kumuokoa mwanaharakati huyo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Chadema, Tumaini Makene amethibitisha taarifa za kupatikana kwa Mdude akisema kwamba, alizungumza naye ingawa ilikuwa kwa shida kutokana na hali yake.

Mdude alitekwa na watu wasiojulikana Jumamosi ya tarehe 4 Mei mwaka huu akiwa ofisini kwake maeneo ya Viwawa katika Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe.

Baada ya Mdude kupatikana watu kadhaa walitoa wito kwa vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa matukio ya utekaji watu, ili kuikomesha desturi hiyo.

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa, kupatikana kwa Mdude kusiwafanye Watanzania kubweteka kwani wasipofanya hivyo huenda matukio kama hayo yakajitokeza tena.

“Pamoja na kufurahia ndugu yetu Mdude Nyangali kurudishwa akiwa hai na kumwombea apone, tusibweteke. Tupaze sauti kutaka Uchunguzi wa matukio haya ya utekaji. Ni rahisi kujisahau na kujipongeza kwa kelele mtandaoni na baada ya miezi kadhaa atachukuliwa mwengine. #UchunguziHuru,” ameandika Zitto.

Aidha, Zitto amewashukuru baadhi ya Watanzania waliopaza sauti zao kwa mamlaka husika wakitaka Mdude apatikane akiwa hai.

“Nawashukuru Watanzania waliosimama pamoja katika kampeni ya #BringBackMdudeAlive kwa njia mbalimbali. Mshikamano dhidi ya UKATILI, udhalimu na ukandamizaji ni silaha. Uchunguzi HURU lazima ufanywe dhidi ya vitendo vya utekaji ambavyo vimeshamiri kwenye utawala wa Awamu ya Tano.”

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, amewashukuru Watanzania walioshiriki kwa namna mbalimbali kupaza sauti zao na kupelekea Mdude kupatikana akiwa hai.

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amevitaka vyombo vya dola kuwachukulia hatua watu waliohusika katika tukio la kumteka Mdude.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Spread the loveWATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

error: Content is protected !!