Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mshirika wa Rais Assaad, afungwa Ujerumani
Kimataifa

Mshirika wa Rais Assaad, afungwa Ujerumani

Eyad al-Gharib
Spread the love

 

MAHAKAMA nchini Ujerumani, imemhukumu kifungo cha miaka minne na nusu gerezani, afisa wa zamani wa Idara ya Usalama wa taifa wa Syria. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Eyad al-Gharib, raia wa Syria, amehukumiwa kifungo na mahakama mjini Koblenzi, Magharibi mwa Ujerumani, baada ya kumtia hatiani katika makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Huu utakuwa uamuzi wa kwanza kutolewa nje ya Syria; wanaharakati wa haki za binaadamu wanasema, uamuzi dhidi ya Eyad (44), “utafungua milango kwa kesi nyingine.”

Afisa huyo wa idara ya usalama wa taifa wa taifa hilo – Syria’s General Intelligence Directorate (GID) – alituhumiwa kutenda makosa hayo, kati ya Aprili 2011 na Septemba 2012.

Eyad anatuhumiwa kukusanya watu waliokuwa wakiandamana kupinga serikali ya Al Asaad, katika mji wa Douma nchini Syria, mwaka 2011 na kisha kuwasagwa hadi kwenye gereza la mahabusu la Al Khatib.

Baada ya kuwafikisha katika gereza hilo, yeye kwa kushirikiana na “watiifu wengine wa serikali ya Asaad,” waliwatesa raia hao wasiokuwa na hatia, hadi wengine kufariki dunia.

Mahakama imeelezwa na upande wa mashitaka kuwa Eyad aliwachukua waandamanaji wapatao 30 waliokuwa wakipinga serikali hadi kwenye gereza la siri karibu na mji wa Damascus.

Gereza hilo ambalo linajulikana kama tawi Na. 251 la Asaad ndilo lililokuwa likitumika kama kituo cha mateso, ubakaji, vitendo vya ngono na udhalilishaji.

Eyad alikamatwa mwaka 2019 nchini humo, baada ya kutambuliwa na wahanga aliowatesa ambao wengi wao, wamekimbilia Ujerumani kuomba hifadhi ya ukimbizi.

Mwaka 2012 Eyad alikimbia kutoka Syria kwenda Uturuki ambako aliishi kwa mwaka mmoja. Kabla ya Kwenda Ujerumani, aliishi Ugiriki hadi mwaka 2018 kabla ya kukamatwa nchini Ujerumani mwaka 2019.

Eyad al-Gharib

Mwingine aliyekamatwa na Eyad, ni afisa wa zamani wa ngazi ya juu katika Idara ya usalama wa taifa ya Syria (GID), Anwar R, ambaye kesi yake, inasikilizwa pia mjini Koblenz.

Katika kusikiliza kesi hiyo, waendesha mashitaka wa Ujerumani walitumia kanuni za mamlaka ya sheria za kimataifa, ambayo inaruhusu uhalifu wa kivita uliofanywa na wageni kushitakiwa katika nchi zingine.

Kesi dhidi ya Anwar bado inaendelea na uamuzi unatarajiwa kutolewa Oktoba mwaka huu.

Afisa huyo mwenye umri wa miaka 58 alikuwa moja ya mabosi wa Eyad. Anakabiliwa na mashitaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa kuratibu ukatili dhidi ya wafungwa karibu 4,000 kwenye jela ya Al Khatib kati ya mwaka 2011 na 2012 na kusababisha vifo vya watu 58.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!