Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mshindi UVCCM adaiwa kutoa rushwa ya nyama
Habari za Siasa

Mshindi UVCCM adaiwa kutoa rushwa ya nyama

Shaka Hamidu Shaka, Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)
Spread the love

UCHAGUZI unaoendelea ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) umezidi kugubikwa na vitendo vya rushwa, vitisho, matusi ya nguoni na kupigana ngumi hatua inayosababisha kukosekana amani, anaandika Moses Mseti.

Vitendo hivyo viliibuka jana katika uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Nyamagana jijini Mwanza na kusababisha baadhi ya wajumbe kuandamana.

Vijana hao waliandamana hadi ofisi za CCM mkoa kupinga matokeo ya mshindi wa uchaguzi huo wilaya ya Nyamagana kwa kile walichodai kwamba uligubikwa na rushwa na vitisho.

Mwanahalisi online, iliwashuhudia vijana hao wakitoka nje ya ukumbi huo na kuandamana hadi ofisi za CCM mkoa majira ya saa nane mchana (jana) huku wakimtuhumu Katibu wa chama hicho mkoa kushindwa kuwasikiliza.

Uchaguzi huo ambao ni wa marudio ulifanyika jana Septemba 27 kwenye ukumbi wa Ghand huku mshindi, Philipo Magori aliyepata kura 163 akionekana kubebwa waziwazi na viongozi wa wilaya hiyo na kumshinda mgombea mwenza, Yusufu Ludimo aliyepata kura 135.

Awali uchaguzi huo ulipofanyika Septemba 23 mwaka huu katika ukumbi wa Kishimba Mtaa wa Uhuru ambapo Ludimo alipata kura 167 Magori kura 109 na mgombea wa tatu Hasan Mambosasa akiambulia kura 33 huku wajumbe 24 wa kata ya Mahina wakizuiwa kupiga kura.

Wakitoa malalamiko yao kwa Katibu wa UVCCM mkoa wa Mwanza, Mariam Amir baada ya kuandamana, baadhi ya wajumbe hao akiwemo Ludimo walisema Magori ameshinda kwa matakwa ya viongozi wa wilaya hiyo.

Walieleza kwamba, siku moja kabla ya uchaguzi wa marudio rushwa ilikuwa ikitolewa waziwazi ikiwa Magori kupigiwa kampeni mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya hiyo aliyemaliza mda wake, Hussein Khim.

“Tunao ushahidi siku moja kabla ya uchaguzi wa marudio baadhi ya wajumbe waliitwa katika ukumbi wa baa ya JM Igoma wakapewa nyama na fedha,” alidai Mfungo Deus kwa niaba ya wenzake.

Wajumbe hao walisema katika uchaguzi wa awali kabla ya kuhesabu kura Ludimo kila alipokuwa akienda aliwekwa chini ya ulinzi wa Green Gurd, lakini Magori aliachwa huru akifanya kampeni ukumbini jambo ambalo lilianza kuwapa wasiwasi.

“Baada ya kupiga kura na kuhesabiwa Ludimo alishinda, lakini kutokana na viongozi wa wilaya akiwemo Katibu Odilia Batholomeo kumbeba shemeji yake Magori, uchaguzi uliahirishwa na kupangwa kufanyika leo (juzi), baadhi ya wajumbe hatukukubaliana na maamzi hayo,” alieleza Deus kwa niaba ya wenzake.

“Sikubaliani na matokeo hayo na sikuyasaini maana kulikuwa na vitisho vya meseji (sms) ambazo tunazo kama ushashidi, baadhi ya wajumbe kupigiwa simu za vitisho na wengine kutukanwa hadharani wakati wakiingia ukumbini na tayari nimeandika barua ya kupinga matokeo hayo katika ngazi ya mkoa,” alieleza Ludimo.

Kwa mujibu wa maelezo ya wajumbe hao kwa Amir, walidai Septemba 25 mwaka huu kabla ya uchaguzi wa marudio Magori alinunua ng’ombe ambaye Khim aliwaeleza baadhi yao wakati akimfanyia kampeni kuwa ni kwa ajili kitoweo cha sherehe baada ya kutangazwa mshindi.

Katibu wa UVCCM mkoa Amir alisema kweli alipokea malalamiko ya vijana hao na kudai uchaguzi wa UVCCM Nyamagana imegubikwa rushwa, vitisho vya watendaji na viongozi ambao wamekuwa wakipanga safu za watu wanaowataka kwa maslahi yao binafsi.

“Hata wajumbe 24 wa Kata ya Mahina waliozuiwa kupiga kura ni wajumbe halali nashangaa kwa nini walizuiwa. Mkoa tulitoa wasimaizi wawili Eva Makune (Katibu Msaidizi wa UVCCM mkoa) na Abel Mahenge Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji, tutaitisha vikao kupitia malalamiko hayo,” amesema Amir.

Amir aliwaomba vijana wa Nyamagana kuwa na uvumilivu wakati vikao vikipitia malalamiko yaliyowasilishwa na kwamba taarifa zitatolewa baada ya vikao hivyo kutoa maamzi.

Taarifa za ndani kutoka chama hicho tawala, zinaeleza kuwa miongoni mwa watu walioratibu mbinu hizo za kuchakachua matokeo ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Marry Tesha na Mbunge wa jimbo hilo, Stanslaus Mabula ili kujitengenezea safu katika uchaguzi mkuu mwaka 2020.

Kwa kipindi kirefu baadhi ya vijana wa CCM wamekuwa wakimtuhumu mbunge huyo kwa kushindwa kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 – 2020, hatua ambayo wanadai inaweza kusabisha jimbo hilo kurudi kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Vijana hao wamekuwa wakidai kwamba walimpigia kura mbunge huyo kutokana na kupitishwa na chama chao huku wakisema endapo kama chama hicho kitamrudisha katika uchaguzi ujao hawatamuunga mkono ni bora wakakihama chama.

Mkuu wa Wilaya alipotafutwa kuzungumzia tuhuma hizo, kwa njia ya simu ya mkononi alipokea kabla hajaelezwa dhumuni la kupigiwa simu alikata na hata alipopigiwa kwa mara nyingine hakupokea simu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!