May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mshindi Miss East Africa kujinyakulia gari la milioni 110

Spread the love

 

MSHINDI wa mashindano ya Miss East Africa 2021, anatarajia kujinyakulia gari jipya aina ya Nissan x Trail, toleo la mwaka 2021 lenye thamani ya Sh.110 milioni. Anaripoti Mwanaharusi Abdallah, TUDARCo … (endelea).

Mashindano hayo yatafanyika tarehe 26 Novemba 2021, jijini Dar es Salaam yakishirikisha nchi 16 za ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi Jumanne tarehe 31 Agosti 2021, Rais wa mashindano hayo kwa Afrika Mashariki (Miss East Africa Beauty Pageant ), Rena Callist amesema, jumla ya Sh.146 milioni, zitatumika kwa zawadi kuanzia mshindi wa kwanza hadi wa tatu.

Rena Callist

Rena alisema, mshindi wa pili atapata fedha taslim Sh.11 milioni na mshindi wa tatu atajipatia fedha taslim Sh.5 milioni katika mashindano hayo yanayoandaliwa na Rena Events Limited

Alizitaja nchi ambazo tayari zimethibitisha kushiriki; ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, South Sudan, Ethiopia, Elitrea, Djibouti, Somalia, Malawi, Visiwa vya Seychelles, Comoros, Madagascar, Reunion na Mauritius.

Rena alisema, mashindano hayo yanatarajiwa kurushwa moja kwa moja na kuangaliwa na watazamaji wengi duniani kupitia telelevision ambapo Tanzania itafaidika na mashindano hayo moja kwa moja kwa kutangaza vivutio vya utalii, fursa za uwekezaji wa biashara pamoja na utamaduni kwa ujumla.

error: Content is protected !!