Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mshindi mashindano ya Qur’an Tanzania atoka Niger
Habari Mchanganyiko

Mshindi mashindano ya Qur’an Tanzania atoka Niger

Spread the love

 

JIBRIL Omar Hassan kutoka nchini Niger, ndio mshindi wa kwanza mashindano makubwa ya Qur’an Afrika 2021, yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al – Hikma Foundation, Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mshindi huyo aliyepata alama 99.83, amepewa zawadi ya Sh. 20 Mil, vocha ya Sh 1 Milioni itakayomuwezesha kuingia katika duka lolote la GSM kuchukua bidhaa aipendayo pamoja na cheti cha ushindi.

Matokeo hayo yametangazwa leo tarehe 25 Aprili 2021, katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maelfu ya Wislam pia wasio Waislam.

Mshindi wa pili kwenye mashindano hayo ni Hassan Ibrahim Hamad kutoka Sudan aliyepata alama 99.41. Zawadi aliyopewa ni Sh. 12 Mil, vocha ya Sh. 700,000 itakayomuwezesha kuingia duka lolote la GSM kuchukua bidhaa ya kiwango hicho cha fedha Pamoja na cheti cha ushindi.

Nafasi ya tatu imechukuliwa na Sadale Khalid kutoka Ivory Cost ambaye amepata alama 99.25. Mshindi huyo amezawadiwa Sh. 7.5 Mil, vocha ya Sh. 500,000 itakayomuwezesha kuingia duka lolote la GSM kuchukua bidhaa ya fedha hiyo pamoja na cheti cha ushindi.

Mshindi wa nne ametoka Tanzania Bara, ni Omar Abdallah Sadi ambaye amepata alama 99.16. Amezawadiwa Sh. 5 Mil, vocha ya Sh. 200,000 itakayomuwezesha kuingia duka lolote la GSM kuchukua bidhaa ya kiwango hicho cha fedha, pia amewewa cheti cha ushindi.

Nafasi ya tano imekwenda Nigeria ambapo mshiriki Mustafa Ali amepata alama 99.00. Mshindi huyo amepewa Sh. 3 Mil, vocha ya Sh 200,000 ya kuingia katika maduka ya GSM kuchukua bidhaa ya pesa hiyo pamoja na cheti ushindi.

Mashindano hayo ya 21, yanayodhaminiwa na taasisi mbalimbali zikiongozwa na Benki ya Watu wa Wanzibar (PBZ), yamehudhuriwa na washindani 23 kutoka nchi 21 za Afrika.

Katika mashindano hayo, mgeni rasmi alikuwa Dk. Hussein Mwinyi, Rais wa Zanzibar huku Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu akiwa mgeni maalum.

Wageni wengine mashughuri waliohudhuria mashindano hayo ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubei; Mufti wa Zanzibar, Sheikh Al Kaabi; Abubakar Kunenge, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam; Hamad Masauni, Naibu wa Waziri wa Fedha na Mipango; Abdallah Ulega, Waziri wa Mifugo na uvuvi na Omari Kumbilamoto, Meya wa Jiji la Dar es Salaam

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa vya ujenzi, samani kwa shule ya msingi Sinyaulime, Chuo cha FDC Morogoro

Spread the loveBENKI ya NMB imekabidhi vifaa vya ujenzi kwa shule ya...

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

error: Content is protected !!