Spread the love

MJASIRIAMALI mkazi wa Same mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania, Ally Athuman Mnyone ameibuka na ushindi wa pikipiki ya miguu mitatu maalumu kwajili ya kubebea mizigo kwenye Kampeni ya bonge la mpango inayoendeshwa na Benki ya NMB. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Akizungumza mara baaya ya kupata zawadi hiyo mshindi huyo ameonesha kufurahishwa na zawadi hiyo na kusema pikipiki hiyo itamsaidia kumuinua kiichumi.

Mjasiriamali huyo amewataka wateja wenzake kuendelea kuweka fedha zao katika benki hiyo huku akiwaaminisha jambo hilo linafanywa kwa uadilifu na kwamba hakuna udanganyifu wa aina yeyote ile.

“Nataka niwaaminishe watu kwamba hii kampeni ya bonge la mpango haimpendelei mtu yeyote na wala haina udanganyifu wowote, mimi watu hawa hawanijui wala mimi siwajui lakini leo hii nimeibuka na ushimdi huu ambao kwangu mimi naona ni hatua kubwa nimeipiga kimaisha,” amesema Mnyone

Naye Dismas Prosper ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini amesema kampeni hiyo inatokana na faida waliyoitengeneza kama benki kurudisha sehemu ya faida kwa wateja wao.

Meneja huyo amesema benki hiyo ilitenga zaidi ya Sh.300 milioni kama zawadi zikiwemo pikipiki 50 za miguu mitatu za mizigo aina ya Skymark.

Kampeni hiyo inamuwezesha Mtanzania yeyote aliyekuwa na akaunti ya NMB au alifungua akaunti mpya na akajiwekea angalau shilingi laki moja anaweza kuibuka mshindi wa zawadi.

“Kampeni ya bonge la mpango awamu ya pili ambayo imelenga sana kuhamasisha wananchi na Watanzania kwa ujumla kuweka akiba kwenye mazingira salama hasa wakitumia benki ya NMB,” amesema Meneja huyo.

Amesema kila wiki katika kipindi cha miezi mitatu tulichokuwa tunacheza hii kampeni ya bonge la mpango toka mwezi wa kumi wateja 10 walikuwa wanajishindia fedha taslimu na wateja wawili walikuwa wanajipatia pikipiki hizi za mizigo za miguu mitatu aina ya skymark lakini kila mwisho wa mwezi kampeni hii iliyokuwa ikichezwa wateja watatu walikuwa wanaondoka na pikipiki za aina hii.

Aidha, meneja huyo wa kanda amewahamasisha Watanzania kuendelea kujiwekea akiba kwenye akaunti zao ndani ya benki hiyo ili waweze kupata nafasi kushinda zawadi mbalimbali kutoka katika benki hiyo.

Jumla ya zawadi zenye thamani ya Sh.300 milioni zimetolewa na benki ya NMB kwajili ya wateja wao ambapo zawadi hizo ni pamoja na pikipiki za miguu mitatu kwajili ya kubebea mizigo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *