January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mshery achukua mikoba ya Diarra Yanga

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Yanga imemtangaza rasmi mlinda mlango Aboutwalib Hamidu Mshery kama usajili mpya ndani ya klabu hiyo akitokea kwenye kikosi cha mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mshery ametangazwa na klabu hiyo hii leo tarehe 29, Desemba 2021, ambaye anakuja kuchukua mikoba ya Djigui Diarra ambaye amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 28 wa timu ya taifa ya Mali kitakachoshiriki michuano ya kombe la Mataifa Afrika (AFCON).

Michuano hiyo ya Afcon inatarajia kuanza kutimua vumbi tarehe 9, Januari 2022 nchini Cameroon ambapo Mali imepangwa kundi kundi F, sambamba na timu za Taifa za Gambia, Mauritania na Tunisia.

Mlinda mlango huyo amesajiliwa mara baada ya siku ya jana uongozi wa klabu ya Yanga, sambamba na benchi la ufundi likiongozwa na kocha mkuu Mohammed Nabi kuonekana kumfuatilia kinda huyo kwa njia ya televisheni, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliowakutanisha Mtibwa Sugar dhidi ya Coastal Union ya jijini Tanga.

Kwenye mchezo huo Mshery aambaye alikuwa kwenye lango la Mtibwa Sugar alionekana kufanya kazi kubwa kiasi cha kuisadia timu yake kuondoka na pointi tatu kwa kushinda ugenini kwenye dimba la Mkwakwani kwa ushindi wa mabao 2-1.

Mara baada ya usajili huo mlinda mlango huyo amoja kwa moja anakwenda kuwa sehemu ya mchezo unaokuja wa Ligi utakaopigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa, Dar es Salaam, ambapo Yanga itakuwa inawakalibisha Dodoma Jiji FC.

Mchezo huo utapigwa Ijumaa ya tarehe 31 Desemba 2021 majira ya saa 1 kamili usiku.

 

error: Content is protected !!