September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mshauri wa Rais anaswa akila uroda na mwanaye

Spread the love

SERIKALI ya Dk. Ali Mohammed Shein imezama kwenye aibu, ni baada ya mshauri wake Dadi Faki Dadi kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ngono na mwanaye, anaandika Pendo Omary.

Faki alikuwa Mkuu Mkoa wa Kaskazini Pemba lakini baada ya kukosa nafasi hiyo katika ngwe ya pili ya Dk. Shein, aliteuliwa kushika nafasi hiyo ya ushahuri kwa rais hususan masuala ya yanayohusu Pemba.

Mshauri huyo amekamatwa kwa tuhuma za kufanya ngono na mtoto wake wa kambo (mtoto wa mkewe) mwenye umri wa miaka 21.

Mwanasiasa huyo maarufu visiwani humo alikamatwa mbele ya mkewe na baadhi ya wanafamilia juzi katika nyumba ya wageni ya Executive, jirani na Makao Makuu ya Uhamiaji Zanzibar, eneo la Kilimani mjini Unguja na kupelekwa katika kituo cha Polisi Mwembemadema.

Mkadam Khamis, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi amethibitisha kushikiliwa kwa Dadi na polisi kwa muda kabla ya kumwachia kwa dhamana wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

“Tunaendelea kufanya uchunguzi. Iwapo tutabaini ametenda kosa tutampeleka katika vyombo vya sheria,” amesema Khamis.

Aidha, picha za video ambazo zinaendelea kusambazwa katika mitandao ya kijamii zinamuonesha Dadi akishambuliwa kwa maneno makali kutoka kwa mkewe na watu waliomkamata.

error: Content is protected !!