May 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mshambuliaji mpya Yanga aibuka mchezaji Bora mwezi Julai

Waziri Junior

Spread the love

MSHAMBULIAJI wa zamani wa klabu ya Mbao FC ya Mwanza, Waziri Junior ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwezi Julai katika msimu wa 2019/20 baada ya kuwabwaga wachezaji Peter Mapunda wa Mbeya City na Obrey Chirwa wa Azam FC. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mshambuliaji huyo ambaye hivi karibuni amejiunga na klabu ya Yanga kwa mkataba wa miaka miwili alimaliza Ligi Kuuu akiwa na mabao 13 licha ya klabu yake ya Mbao FC kushuka daraja.

Katika michezo sita ya Ligi Kuu Tanzania Bara waliocheza klabu ya Mbao FC kwa mwezi Julai, walifanikiwa kushinda michezo mitano na kwenda sare mechi moja, huku mshambuliaji huyo akipachika mabao matano na kutoa pasi moja ya goli.

Baada ya klabu yake hiyo kushuka daraja, mshambulijai huyo ataonekana tena kwenye Ligi hiyo akiwa na klabu yake mpya ya Yanga ambayo ataanza maisha yake mapya ya soka.

Fred Minziro

Katika hatua nyingine kamati ya Tuzo ya Ligi Kuu, imemchagua kocha wa klabu hiyo Fred Felix Minziro kuwa kocha bora wa mwezi Julai, 2020 baada ya kuwashinda makocha Amri Said wa Mbeya City na Aristica Cioaba wa Azam FC.

Minziro ameshinda tuzo hiyo baada ya kuingoza Mbao FC katika michezo sita ya mwisho na kufanikiwa kushinda mechi tano na kwenda sare mchezo mmoja na kuipeleka timu hiyo kwenye mtoano (Play off).

error: Content is protected !!