August 12, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mshahara wamponza bosi TIC

Spread the love

RAIS John Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurungezi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Juliet Kairuki kwa kile alichokiita “Julieth Kairuki amekua hachukui mshahara wa serikali tangu alipoajiriwa mwezi Aprili 2013, anaandika Pendo Omary.

Taarifa iliyotolewa leo na Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, inasema utenguzi huo umefanyika tangu tarehe 24, Aprili mwaka hu na kwamba kitendo cha Kairuki kutochukua mshahara wake kinazua maswali mengi.

Hata hivyo taarifa hiyo inasema endapo Kairuki atakuwa tayari kufanya kazi na serikali atapangiwa kazi nyingine.

Kairuki aliteuliwa tarehe 12 Aprili, 2013 na Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kushika nafasi hiyo iliyoachwa na mtangulizi wake Ole Naiko kustaafu.

Kabala ya kuteuliwa kuongoiza kituo hicho Kairuki alikuwa Meneja Mkuu wa Idara ya Benki na Huduma za Fedha katika Chama Cha Mabeki Afrika Kusini.

Taarifa zilizo wahi kuandikwa na gazati la MAWIO lililofutwa na serikali , zinasema tangu Kairuki aajiriwe na serikali aligoma kuchukua mshahara wake akitaka nyongeza zaidi kutoka Sh.5 Milioni hadi Sh. 18 Milioni walizokubaliana na mteuzi wake, Rais Kikwete ambapo wakati akifanya kazi Afrika Kusini alilipwa takribani Sh. 35 milioni.

Hata hivyo, vyanzo vya gazeti hilo kutoka TIC vilidai kwamba Licha ya Kairuki kugoma kupokea mshahara huo, alijiidhinishia posho kubwa zilizozidi hata kiwango cha mshahara aliopaswa kupoke kwa ajili ya safari zisizo na tija za mara kwa mara nje ya nchi.

error: Content is protected !!