September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mseveni avuruga mabalozi

Spread the love

MABALOZI kutoka nchi za Ulaya, Marekani na Canada jana walisusa sherehe za kuapishwa Yoweri Mseveni, Rais wa Uganda kwa madai ya kiongozi huyo kuishutumu Mahakama ya Kimataifa ya Uhallifu wa Kivita (ICC) pamoja na kuwepo kwa rais wa Sudani Omar Al Bashir anayetafutwa na mahakama hiyo, anaandika Wolfram Mwalongo.

Mseveni ameapishwa jana kuwa rais wa awamu ya tano mfulizo tangu 1986. Akitoa hotuba katika sherehe hizo alisema, ICC ni ya watu wasio na maana na hawezi kuiunga mkono, kauli hiyo ilisababisha mabalozi hao kuondoka.

Aidha Mseveni ameapishwa huku chama cha upinzani cha Forum For Democratic Change (FDC) kikiendelea kupinga ushindi wake .

Mei 11 mwaka huu FDC kilimwapisha Kiiza Besigye, aliyekuwa mgombea wake wa urais na muda mchache baadaye alikamatwa na polisi.

error: Content is protected !!