May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mseven kuapishwa leo, Rais Samia kuhudhuria

Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekwenda nchini Uganda, kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo, Yoweri Museveni. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Samia, ameondoka asubuhi ya leo Jumatano, tarehe 12 Mei 2021, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Sherehe za kuapishwa kwa Mseven, inafanyika leo Jumatano, Uwanja wa Kololo jijini Kampala.

Museveni anaapishwa kuendelea na uongozi wake aliouanza mwaka 1984, baada ya kushinda kiti cha Urais wa Uganda, kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 14 Januari 2021.

Yoweri Museveni

Katika uchaguzi huo, Museven alitangazwa mshindi baada ya kupata asilimia 58.6 ya kura huku aliyekuwa mpinzani wake wa karibu, Robert Kyagulanyi maarufu ‘Bob Wine’ akipata asilimia 34.8 ya kura.

error: Content is protected !!