March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

MSETO kuiponza Tanzania Jumuiya ya Afrika Mashariki

Flugence Massawe, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC)

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania inaweza kuingia katika mgogoro katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kama haitatii maagizo waliyopewa na Mahakama ya Afrika Mashariki ya kulifungulia gazeti la MSETO linalotolewa na Kampuni ya Hali Halisi Publishers baada ya kushinda kesi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Gazeti la MSETO lilifungiwa na Serikali kwa Agosti 10, 2016 kwa madai ya kukiuka kifungu cha 25 cha sheria ya magazeti, lakini Mahakama ya Afrika Mashariki iliyopo jijini Arusha Juni 21, mwaka huu.

Wakili Projest Masawe aliyekuwa anasimamia kesi hiyo katika Mahakama ya Afrika Mashariki, amesema serikali inatakiwa kufuata maagizo yaliyotolewa na mahakama hiyo ya kutengua agizo la gazeti hilo kufungiwa, kinyume na hapo watarudi mahakamani na wakiendelea kukaidi nchi itaingia matatizo.

“Tunaamini Serikali wana taarifa ya hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Afrika Mashariki na ndiyo maana wameonesha nia ya kukata rufaa, lakini wamekaa kimya bila kutekeleza agizo.

“Baada ya muda kupita tunarudi mahakamani kuomba shauri ya kuishinikiza Serikali ilifungulie mteja wetu aendelee na uzalishaji wa gazeti. Wakiendelea kukaidi watakuwa wamevunja kanuni za Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kutekeleza mahakama hiyo,” amesema Masawe.

Wakili Masawa amesema kama Serikali ikiendelea kukaidi hukumu hiyo ya Mahakama ya Afrika Mashariki kuna uwezekano wa kuwekewa vikwazo katika baadhi ya mambo wanayoshirikiana katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers, Saed Kubenea amesema kumekuwa na ucheleweshwaji wa haki hasa katika kesi zinazohusu vyombo vya habari pale vinapofungiwa na serikali kwa sababu zao ambazo zinakuwa kinyume na sheria.

Kubenea amesema kutokana na Serikali kukaa kimya baada ya hukumu hiyo wamedhamilia kurudi tena mahakamani kuomba oda ya itakayoruhusu gazeti lirudi mtaani, maana wameshindwa kutengua agizo lake la kufungia gazeti.

 

error: Content is protected !!