August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msemaji wa White House ya Trump aachia ngazi

Sean Spicer, Msemaji wa Rais wa Marekani

Spread the love

MSEMAJI wa rais wa Marekani, Donald Trump amejiuzulu kufuatia uteuzi wa rais wa mkurugenzi mpya wa mawasiliano nchini humo, anaandika Catherine Kayombo.

Sean Spicer, amejiuzulu kwa kutofurahishwa na mabadiliko hayo ya uongozi katika idara ya mawasiliano, akidai kuwa kuwepo kwa mkurugenzi wa mawasiliano katika Ikulu ya White house kutaleta utata katika utendaji kazi wake.

Spicer hajaridhishwa na uteuzi wa Anthony Scaramucci, mfadhili wa kampuni ya Wall Street kuwa mkurugenzi wa idara ya mawasiliano.

Amefananisha mabadiliko hayo na uwepo wa wapishi wengi jikoni na kwamba kunaweza sababisha kuharibu mapishi.

Msemaji huyo wa zamani amekuwa akimtetea rais Trump na kuvishutumu vyombo vya habari kuwapotosha Wamarekani kuhusu uongozi wa Trump.

Vikao vyake na wanahabari vimekuwa maafuru na mara nyingi huzuia mijadala ya mawazo kati ya wanahabari hasa wale wasiokubaliana na uongozi wa Trump.

Aidha, Trump amemshukuru Spicer kwa kazi aliyoifanya hasa kumtetea mbele ya wanahabari nchini humo.

Amekuwa akimtetea rais hata katika madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka uliyopita.

error: Content is protected !!