Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msekwa ataja sababu Nyerere, Karume kufanya siri makubaliano ya Muungano
Habari za SiasaTangulizi

Msekwa ataja sababu Nyerere, Karume kufanya siri makubaliano ya Muungano

Spread the love

SPIKA wa Bunge mstaafu, Pius Msekwa, amesema Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume, waliendesha makubaliano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa siri, ili kukwepa hujuma kutoka kwa watu wasioafiki suala hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma.(endelea).

Mzee Msekwa ametaja sababu hiyo leo Jumanne, tarehe 26 Aprili 2022, jijini Dodoma, katika maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya muungano huo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango.

Spika huyo mstaafu amesema Nyerere aliyekuwa Rais wa Tanganyika na Karume, aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, walikubaliana mapema juu ya suala hilo ili kulinda jitihada zao zisije zikahujumiwa.

“Jambo ambalo wengi hawalijui ni usiri mkubwa wa mazungumzo baina ya marais hao wawili ulivyokuwa, usiri mkubwa sana wa mazungumzo baina ya marais hao kabla hawajafikia makubaliano hayo yaliendeshwa kwa siri kubwa sababu na umuhimu wa kuwepo kwa siri hiyo ilikuwa hofu kubwa iliyokuwepo,” amesema Mzee Msekwa.

Mzee Msekwa amesema “kwamba endapo mazungumzo hayo yangejulikana mapema, maadui wa muungano wanaweza wakatengeneza njama za kuhujumu jitihada hizo ili zisiweze kufanikiwa lengo. Usiri huo ulikuwa kwa ajili ya kulinda jitihada zao zisije zikahujumiwa.”

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini Tanzania, amesema hata siku Mwalimu Nyerere anatoka Dar es Salaam, kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kusaini hati ya makubaliano na Karume, alifanya siri kiasi cha Gazeti la TANU la Nationalist liliandika nakwenda visiwani humo kwa ziara ya kirafiki.

“Ukweli huo ulikuja kufichuka jioni, baada ya mambo kukamilika ndiyo taarifa ilitoka Ikulu ya Zanzibar kwa kifupi, ikisema Rais Nyerere na Rais Karume leo wamesaini mkataba wa makubaliano ya kuunda muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, makubaliano hayo sharti yaridhiwe na Serikali zote mbili na mabunge ya pande zote mbili.,” amesema Mzee Msekwa.

Amesema muungano ulizaliwa Jumapili ya tarehe 26 Aprili 1964, baada ya serikali na mabunge ya pande zote mbili kuridhia makubaliano hayo, ambayo yalimfanya Mwalimu Nyerere kuwa Rais wa Tanzania na Karume kuwa Makamu wa Rais.

Baada ya muungano huo kuzaliwa, Bunge la Tanganyika likavunjwa na kuanzishwa Bunge la Tanzania, pamoja na kutungwa kwa katiba ya mpito.

Amesema sherehe za muungano hazikufanyika kipindi hicho kutokana na muda wa maandalizi kuwa mchache, ambapo mwaka mmoja baadae maadhimisho yalifanyika.

Mzee Msekwa amesema, katika hati hiyo ya makubaliano, kulikuwa na mambo ya muungano 11, lakini baadae yaliongezeka na kufikia 22 yaliyokuwepo hivi sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!