June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

MSD yapata muarobaini wizi wa dawa

Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kulia), akimuelekeza jambo Mwanahabari aliyetembelea banda la MSD katika maonyesho hayo

Spread the love

BOHARI Kuu ya Dawa nchini (MSD), imepata muarobaini ya kuwadhibiti wezi wa dawa za serikali kwa kuziwekea nembo maalum. Anaandika  Jimmy Mfuru … (endelea)

Tayari zoezi hilo lishaanza ambamo hadi sasa dawa 42 zishawekewa nembo hizo zijulikanazo kama (GOT), na jitihada bado zinaendelea kwa dawa nyingine.

Aidha,  jitihada bado zinaendelea kufanywa na bohari hiyo kuendelea kuziweka nembo zaidi dawa nyingine za kawaida ambayo jumla yake ni 630,na zile za mradi msonge jumla yake 613.

Hayo yalibainishwa leo  Jijini Dar es Salaam na Afisa Uhusiano Mkuu wa MSD Etty Kusiluka katika mahojiano na Mwanahalisionline katika wiki ya maonyesho ya  Utumishi wa Umma yanayoendelea viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

“MSD bado inaendelea kuweka dawa za serikali nembo ili kudhibiti wizi wizi na tumeanza na aina hizo 42 bado tunaendelea kuweka nyingine zilizobakia”,amesema Kusiluka.

Amezitaja moja ya dawa hizo zilizowekewa nembo ni Magnesium,Amoxilin,Ciproflaxin,paracetamol,Dixlophenac,  Clotromoxin na nyinginezo.  

Ameongeza kuwa wamejipanga kusogeza huduma karibu na wananchi kwa wananchi wanampango wa kufungua maduka yao kwenye mikoa minne.

Ikiwa lengo ni kuziondolewa usumbufu hospitali kuagiza dawa kwenye ofisi ya kanda mara zinawaishia ghafla na maduka hayo yatakuwa ndani ya hospitali au karibia na hospitali.

Ametaja mikoa ambayo wanaanzia kufungua maduka hayo  ni Mbeya,Dar es Salaam,Mwanza na Arusha ambamo yatakuwa yanafanyakazi saa 24.

“Tumeamua kusogeza huduma karibu na jamii kwa kufungua maduka katika mikoa hiyo aidha,ndani ya hospitali au karibu na hospitali kuzirahisishia kuzinunua pindi wanaishiwa na dawa kabla ya kuziagiza”,anasisitiza Kusiluka

error: Content is protected !!