July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

MSD yaingia mtandaoni

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda wa MSD, Edward Terry akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maboresho ya huduma zao

Spread the love

BOHARI ya Dawa nchini (MSD), imeboresha zaidi huduma zake ili kumpatia mteja taarifa zinazomuhusu kwa kuziweka wazi katika tovuti yake, ambapo zinapatikana muda wote.  Anaandika Sarafina Lidwino… (endelea)

Taarifa hizo zikiwa ni, mali inayopatikana ghalani, kiasi cha fedha kilichopo katika akaunti zao, fomu za marejesho na orodha ya bidhaa zake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kaimu Mkurugenzi huduma kwa wateja na shughuli za kanda, Edward Terry, amesema shughuli za MSD ni kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa, vifaa na vitendanishi vya maabara kwenye hospitali, vituo vya afya, zahanati na umma na taasisi zilizoainishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Terry amesema, mpaka sasa MSD inasambaza dawa na vifaa tiba moja kwa moja hadi kwenye hospitali na vituo vya afya na zahanati za serikali kwa nchi nzima.

“Ukiona mganga mkuu wa hospitali ya serikali yoyote analalamikia MSD, kwamba hawajasambazi dawa za kutosha au kwamba tumeishiwa dawa, sio kweli- mteja huyo lazima atakuwa na matatizo katika ulipaji,” amesema Terry.

Ameeleza kuwa, taasisi nyingi za afya zimekuwa zikiilalamikia MSD pasipo kujua kinachoendelea. “Sio kwamba dawa zinakuwa hamna, zinakuwepo ila huwezi kuletewa dawa wakati bado una deni kubwa na kwenye akaunti yako huna fedha ya kutosha.

Mfano; mteja anaagiza dawa za bilioni moja wakati kwenye akaunti yake ana laki tano, sasa ukimpa dawa kulingana na fedha yake analalamika, hapo tufanyeje? Amehoji Terry.

Hata hivyo, Terry amewakumbusha wateja wote kuwasilisha mahitaji yao katika ofisi za MSD kabla ya 30 Aprili mwaka huu, pamoja na nyaraka muhimu zinazohitajika ambazo ni pamoja na kivuli cha mpango wa mmanunuzi cha taasisi husika na kiasi cha fedha kilichoidhinisha katika bajeti.

error: Content is protected !!