June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

MSD kusogeza zaidi huduma kwa wananchi

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (aliyesimama) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Spread the love

BOHARI Kuu ya Dawa (MSD), imejipanga kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kufungua maduka kwenye mikoa minne nchini. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani katika mahojiano maalum na MwanaHALISI online yaliyofanyika kwenye viwanja vya Maonyesho ya Utumishi wa Umma Jijini Dar es Salaam.

Amesema, lengo ni kuziondolewa usumbufu hospitali kuagiza dawa kwenye ofisi ya kanda pale zinapoisha na kwamba, maduka hayo yatakuwa ndani au karibu na hospitali. 

Ametaja mikoa ambayo wanaanzia kufungua maduka hayo ni Mbeya, Dar es Salaam, Mwanza na Arusha ambamo yatakuwa yanafanyakazi kwa saa 24.

“Tumeamua kusogeza huduma karibu na jamii kwa kufungua maduka katika mikoa hiyo ndani ya hospitali au karibu na hospitali ili kuzirahisishia kuzinunua pindi wanaishiwa na dawa kabla ya kuzigiza,” amesema Mwaifwani.

Akizungumzia mafanikio amesema, wamepata  muarobaini wa kuwadhibiti wezi wa dawa za serikali kwa kuziwekea nembo maalum.

Na kuwa, tayari  zoezi hilo limeanza ambapo hadi sasa aina ya dawa 42 tayari ziwekewa nembo hizo zijulikanazo kama GOT  na jitihada bado zinaendelea kwa dawa nyingine.

Jitihada zinafanywa ili kuweka nembo hizo katika dawa za kawaida 630 na zile za Mradi Msonge ambazo jumla yake 613.

“MSD bado inaendelea kuweka dawa za serikali nembo ili kudhibiti wizi na tumeanza na aina hizo 42 bado tunaendelea kuweka nyingine zilizobakia,” amesema Mwaifwani.

Amezitaja moja ya dawa hizo zilizowekewa nembo kuwa ni Magnesium, Amoxilin, Ciproflaxin, Paracetamol, Dixlophenac,  Clotromoxin.

error: Content is protected !!