October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msanii Vitalis Maembe ajiunga ACT-Wazalendo, atangaza kugombea Bagamoyo

Spread the love

VITALIS Maembe, Mwanamuziki na Mwanaharakati nchini Tanzania, amesema amejiunga na Chama cha ACT-Wazalendo kwa kuwa chama hicho kina misingi ya  kudai haki  na kujipambanua kwenye ujamaa. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Maembe  amejiunga na chama hicho leo Jumatatu tarehe 29 Juni 2020 na kukabidhiwa kadi na Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa chama hicho, makao makuu ya ACT-Wazalendo, Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Maembe amesema ACT-Wazalendo ni chama chenye sifa anazozihitaji kama vile yeye anavyojipambanua kwenye muziki wake.

Amesema chama hicho kimejipambanua kwenye mapambano ya haki na kutetea wanyonge na kujenga umoja wa Afrika.

Kwa upande wake, Shaibu wakati anampokea Maembe amesema, mwanamziki huyo alijipambanua kwenye mtandao kuwa anahitaji kuendeleza mapambano ya haki kupitia siasa.

Wakati huo huo, Maembe amesema kuwa endapo chama hicho kitampa ridhaa atagombea ubunge Bagamoyo.

error: Content is protected !!