Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Msanii maarufu AKA adaiwa kuuawa kwa risasi
Burudika

Msanii maarufu AKA adaiwa kuuawa kwa risasi

Spread the love

RAPA maarufu nchini Afrika Kusini, Kiernan Forbes ‘AKA’ ameuawa akiwa amesimama nje ya mgahawa mmoja huko Durban jana usiku.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini humo, inadaiwa kuwa magari mawili yalipita na kufyatua risasi muda wa saa 10 jioni kwa saa za huko. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Rapa huyo alitakiwa kutumbuiza katika klabu ya usiku iitwayo YUGO usiku huo wa Ijumaa.

Taarifa ilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii, ikisema kuwa hafla hiyo ilighairiwa kutokana na hali zisizotarajiwa.

Inadaiwa kuwa AKA alipigwa risasi sita, huku mwanaume mwingine naye akidaiwa pia kuuawa kwenye tukio hilo.

Rapa mzaliwa wa Cape Town, aliingia kwenye tasnia hiyo baada ya kuachia wimbo wa Victory Lap kutoka kwenye albamu yake ya kwanza, Altar Ego mwa 2011.

Albamu hiyo ilishinda tuzo kadhaa na mwaka 2021 alitangazwa kuwa msanii bora wa kiume wa mwaka katika tuzo za muziki za Afrika Kusini.

Aliendelea kufanikiwa na albamu yake ya pili Levels mwaka 2014, ikifuatiwa na yake ya tatu, Touch My Blood, mwaka 2018.

AKA alichumbiana kwa muda mfupi na DJ Zinhle na mwaka 2015 walifanikiwa kumpata binti Kairo.

Aidha, msanii huyo alishirikiana na wasanii wa Tanzania Joh Makini katika  wimbo wa Donbother huku Staa Diamond Platnumz akishirikiana naye katika wimbo wa Make me sing.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the loveMAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia...

Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the loveSTAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B,...

Burudika

Mr. Eazi aachia Advice ikiwa ni ujio wa albam mpya

Spread the loveSTAA wa muziki kutoka nchini Nigeria, Mr.Eazi ni gwiji linapokuja suala...

error: Content is protected !!