May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msanii C-Pwaa hatunaye

Spread the love

MSANII wa Bongo Fleva, Ilunga Khalifa ‘C-Pwaa’ amefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 17 Januari 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

C-Pwaa aliyefanya kazi na wasanii kadhaa enzi za uhai wake akiwemo Ngwair (marehemu), Dully Sykes pia kundi la Park Lane, amekutwa na mauti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alipokuwa akipatiwa matibabu kwa siku nne zilizopita.

Tayari wasanii wenzake wa muziki pia maigizo, wamekuwa wakitoa salamu za pole kwa familia, ndugu na jamaa wa C-Pwaa.

Miongoni mwa ma-poroduza aliowahi kufanya kazi na C-pwaa ni pamoja na P Funk Majani ambaye amethibitisha kifo cha msanii huyo.

error: Content is protected !!