September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msani/Diwani ACT-Wazalendo atupwa jela

Clayton Chipando maarufu kwa jina la Baba Levo

Spread the love

MSANII wa kizazi kipya na mwanasiasa wa upinzani nchini Clayton Chipando maarufu kwa jina la Baba Levo, leo tarehe 1 Agosti 2019 amehukumiwa kwenda jela kwa miezi mitano. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Baba Levo ambaye ni Diwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini kweneye Manispaa ya Kigoma Ujiji, mkoani Kigoma kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia ya kumshambulia askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani humo F.8350 PC Msafiri Mponela.

Juma Ramadhani, Katibu wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Kigoma  amethibitisha na kuongeza “bado tunafuatilia hukumu hiyo.”

Kwa mujibu wa mahakamani hao, kifungu kifungu No. 240 cha kanuni ya adhabu Sura ya 16 chapisho la mwaka 2002 ndio lililomtia hatiani Baba Levo.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi, Florence Ikolongo wa Mahakama ya Mwanzo iliyopo Mwandiga na kwamba, hukumu hiyo bila faini.

error: Content is protected !!