January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msama ahudumia vituo 10

Spread the love

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Msama Promotion, Allex Msama leo ametoa msaada wa Sh. 7,000,000 katika vituo 10 vya kulelea watoto yatima vilivyopo jijini Dar es Salaam. Anaandika Sarafina Lidwino… (endelea).

Vituo hivyo ni pamoja na Zaidia (Sinza), Hiyari (Chang’ombe), Malaika (Kinondoni), Maunga (Mkwajuni), Sifa (Bunju), Honorata (Temeke), Chakuwama (Mwenge), Rahman (Magomeni), Umra (Magomeni) na Mwandaliwa (Boko).

Kwa kila kituo Msama ametoa msaada wa unga wa ngano viroba viwili, unga wa mahindi viroba vinne, sukari viroba viwili, ndoo ndogo za mafuta tatu, sabuni paketi nne, chumvi paketi mbili, sabuni ya unga viroba viwili, mafuta ya kupaka paketi tano, dawa ya meno boksi mbili na mchele kilo 50.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zake zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam Msama amesema ametoa msaada huo ili kutimiza ahadi yake kwa wananchi ambapo aliahidi kila atakapoaandaa tamasha pesa zitarudi kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu.

Msama ambaye pia ni mwenyekiti wa uaandaaji wa matamasha makubwa nchini amesema kuwa, misaada hiyo pia ni matunda ya wananchi kutokana na tamasha la kuombea amani lililofanyika Oktoba 4 mwaka huu.

“Natoa rai kwa wananchi waendelee kuguswa, hata tunapoandaa tamasha lingine wajitokeze kwa wingi ili tupate pesa za kutosha kwa ajili ya kuwasaidia watoto hawa ili nao wajione wanakumbukwa na kupendwa licha ya kupoteza wazazi wao,” amesema Msama.

Aidha, Msama amesema anampango wa kutoa misaada hiyo katika mikoa 20 ambapo kwa sasa ameshatoa katika mikoa minne ambayo ni, Shinyanga, Dodoma, Singida na Mwanza.

error: Content is protected !!