October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msalala wapatiwa mikopo ya Sh milioni 138

Spread the love

HALMASHAURI ya Wilaya ya Msalala imetoa mkopo kiasi cha Sh milioni 138 katika Kata ya Bulyanhulu kwa vikundi vitatu vya wanawake, vikundi saba vya vijana na kimoja cha walemavu katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022. Anaripoti Paul Kayanda, Shinyanga… (endelea).

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema katika kongamano la wanawake wa halmashauri lililoandaliwa na Mbunge wa Msalala, Idd Kassim.

Kongamano hilo lililofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Bulyanhulu, lililenga kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani.

Mjema amevitaka vikundi vya wanawake na makundi mengine yanayonufaika na mkopo huo kutumia fursa hiyo vizuri kwa kufanya uwekezaji na biashara zenye tija.

Amesema mikopo hiyo itawasaidia kuongeza mitaji na kiwango cha ajira na kwamba awali walifanya biashara ndogondogo lakini wakiwa wengi watafanya biashara kubwa zaidi.

“Kwa mfano maeneo yenu ya kilimo Msalala, mnaweza kupanua wigo kwa kulima mazao ya biashara na chakula kwa kutumia mkopo huo, pamoja na biashara kubwa kwenye maeneo muhimu,” amesema Sophia.

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama, Charles Fussi kwa kufanikisha zoezi la utoaji wa mikopo kwa vikundi vya Wanawake/Vijana na Walemavu.

Amesema mkurugenzi huyo ametekeleza lengo la ya serikali inayowataka wakurugenzi wa halmashauri kutenga fedha na kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu.

Pia alimuagiza mkurugenzi huyo kuongeza idadi ya vikundi ili makundi hayo yanufaike na mpango wa Serikali.

error: Content is protected !!