Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Msako wamiliki wa visima vya maji waja
Habari Mchanganyiko

Msako wamiliki wa visima vya maji waja

Spread the love

SERIKALI kuanza msako wa wamiliki wa visima visivyolipiwa ada ya matumizi ya maji kwa ajili ya kuwachukulia hatua za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 19 Novemba 2018 jijini Dar es Salaam, Afisa Maji Bonde la Wami/Ruvu, Simon Ngonyani amesema watumiaji wa maji wasiofuata taratibu za kisheria, ikiwemo wamiliki wa hoteli 100, vituo vya mafuta 25 na kampuni 11 watafikishwa mahakamani.

“Hawa watu tukiwapelekea mahakamani tunacho wadai ni zaidi ya milioni 200 na kitu, ukiangalia kuna wengine wana madeni yaani mtu ana kisima miaka kumi iliyopita halipi, tuu hadi leo hizo nazo hatutamuacha nazo atalipa zote, baada ya kufanya zoezi zima tutajua tunawadai shilingi ngapi,” amesema Ngonyani.

Akielezea kuhusu ada za matumizi ya maji, Ngonyani amesema sheria inataka wamiliki wa visima kulipa ada hizo ili zisaidie kwenye masuala mbalimbali ikiwemo utafiti wa mwenendo wa maji chini ya ardhi.

“Sheria inasema hata kama umechimba mwenyewe, sheria inasema ulipe ada ya matumizi ya maji hayo ili hiyo ada itumike, kwa mfano inatakiwa kuangalia mwenendo wa maji ndani ya ardhi ikiwemo ubora wa maji. Sababu tuko karibu na bahari hivyo maji ya bahari yanaweza kupanda juu umechimba kisima leo maji mazuri, unashangaa mwaka mmoja au miaka fulani maji yana chumvi,” amesema Ngonyani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!