MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema itaendelea kufanya ukaguzi wa matumizi za mashine za kutolea risiti za kielektroniki (EFD), ili kuhakikisha kila mfanyabiashara anatoa risiti za EFD na kulipa kodi stahiki. Anaripoti Regina Kelvin …. (endelea).
Hayo yalisemwa jana tarehe 31 Julai, 2018 na Kamishna wa kodi za ndani Elijah Mwandumbya alipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika maduka yaliyopo eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mwandumbya aliwataka wafanyabiashara kuacha kutoa sababu ya ubovu wa mashine za EFD kwa kuwa mashine hizo sasa zinafanyakazi vizuri.
“TRA haitakubali mfanyabishara anayeonesha barua kama sababu ya kutokutoa risiti ya EFD, tatizo la mashine lilikwisha, ni wajibu wa wafanyabiashara kutoa risiti,” amesema Mwandumbya.
Kamishna Mwandumbya amesema wafanyabiashara wote wanaostahili kutoa Risiti za EFD wanapaswa kutoa kwa kila mauzo wanayofanya kwani tatizo la mashine lilishashughulikiwa na limekwisha.
Leave a comment