July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msajili wa Vyama “ajifunga kitanzi”

Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, Jaji Francis Mutungi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Spread the love

JAJI Francis Mutungi-Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, amekunjua makucha na kuvitaka vyama vya siasa kuisoma vyema Sheria ya Gharama za Uchaguzi kabla ya kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu kuanza. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Angalizo la Jaji Mutungi linatazamwa kama sawa na “kujifunga kitanzi”, ambapo wachambuzi wa siasa wanahoji kama ataweza kumwengua mgombea atakayepitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiwa atabainika alikiuka sheria hiyo.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari leo, Jaji Mutingi hakukitaja moja kwa moja chama chochote cha siasa, lakini baadhi ya makada wa CCM wanaoomba kuteuliwa kuwania urais, wadaiwa kutumia mabilioni ya fedha zisizo na ukaguzi na hivyo kukiuka sheria hiyo.

Lakini Jaji Mutungi amesema, “mgombea yoyote atakayevunja masharti na sheria ya gharama za uchaguzi, hatateuliwa na chama. Hata chama kikimpitisha, sheria itafata mkondo wake. Tunatumaini Sekretarieti za vyama zitafuata sheria.”

Anafafanua kuwa, “…mgombea akivuka kiwango kilichopagwa na serikali, chama kitawajibika na kutoa ufafanuzi wa kutosha. Sisi tunaona kila kinachoendelea na muda ukifika tutatoa maamuzi.”

Jaji Mutungi amesema, sheria hizo zinaelekeza kuwepo kwa uwazi katika mapato na matumizi ya vyama na wagombea wao kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Kwamba, sheria zinasema; “chama ndicho kitagharamia mchakato wa kura ya maoni na kampeni za uchaguzi, ambapo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, kila chama kinatakiwa kutovuka matumizi ya Sh. 2 billioni.

“Nimeamua leo kutoa ufafanuzi huu kutokana kwamba inaonekana wagombea wengi pamoja na wananchi hawasomi sheria hizi. Pia niwatahadharishe wagombea kujiepusha na vitendo mbalimbali vyovyote vinavyoonekana kuleta hisia za kununua ama kurubuni wapiga kura,” amesema na kuongeza kuwa;

“Kufanya vitendo vilivyokatazwa ndani ya sheria, kutamkosesha mgombea nafasi ya uongozi.”

Aidha, Jaji Mutungi amepiga marufuku vyama vya siasa kuwa na vikundi vya ulinzi na usalama, vinavyochukua jukumu la Polisi au majeshi mengine nchini.

error: Content is protected !!