Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari Msajili wa vyama aitolea uvivu Chadema
HabariHabari za Siasa

Msajili wa vyama aitolea uvivu Chadema

Spread the love

NAIBU Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kishiriki katika mikutano ya vyama vya siasa, ili kuimarisha ushirikiano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Nyahoza ametoa ushauri huo leo Jumatano, tarehe 11 Mei 2022, jijini Dar es Salaam, akizungumza katika kikao cha Baraza Kuu la Chadema, kilichohudhuriwa na watu mbalimbali ikiwemo baadhi ya viongozi wa vyama vingine vya siasa.

Naibu Msajili huyo wa vyama vya siasa, amemtaka Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, aige mfano wa viongozi wengine wa vyama vya siasa walioshiriki mkutano huo.

“Tumeona vyama vya siuasa vingine vimewaunga mkono, wako wengi tu hapa na hii inaonesha ushirikiano mzuri baina ya vyama na kwenye hili mheshimiwa mwentekiti na nyie muendege kwenye vyama vingine wanapofanya, sio waje kwenu tu,” amesema Nyahoza.

Miongoni mwa viongozi wa vyama vya upinzani walioshiriki mkutano huo, ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Babu Juma Duni Haji. Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Katika hatua nyingine, Nyahoza amekitaka chama hicho kufuata matakwa ya sheria na katiba yake, kinapokwenda kufanya maamuzi juu ya ajenda za kikao hicho cha Baraza lake Kuu.

Miongoni mwa ajenda zinazojadiliwa katika kikao cha baraza hilo, ni rufaa za wabunge viti maalumu 19, akiwemo Halima Mdee, waliokata kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema kuwavua uanachama kwa tuhuma za usaliti.

Ajenda nyingine ni, kujadili taarifa ya kamati kuu ya chama hicho kuhusu mfumuko wa bei ya mafuta nchini, uliosababisha kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu na kupelekea ugumu wa maisha kwa wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!