October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Msajili awalima barua TCD, waahirisha kongamano

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi

Spread the love

 

KONGAMANO la haki, amani na maridhiano lililokuwa lifanyike tarehe 21-23 Oktoba 2021, ambalo linaandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) limeahirishwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya TCD iliyotolewa leo Alhamisi, tarehe 7 Oktoba 2021 na Mwenyekiti wa kamati ya ufudi wa kituo hicho, Sheweji Mkote imesema, wameahirisha baada ya msajili wa vyama vya siasa kuwaandikia barua kuwashauri wasogeze mbele kupisha kikoa kati ya msajili, wadau wa siasa na polisi.

Kikao kati ya msajili na wadau wa siasa, kimepangwa kufanyika tarehe 21 Oktoba 2021, jijini Dodoma kikiwa na lengo la kutafuta mwafaka wa namna bora ya kufanya siasa.

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Zitto Kabwe

Mketo amesema, mara baada ya utaratibu kuwekwa sawa, watatoa taarifa ya kongamano hilo litafanyika lini.

TCD inayoongozwa na Mwenyekiti, Zitto Kabwe inaundwa na vyama vyenye wabunge, wawakilishi na madiwani angalau watatu ambavyo ni; CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na ACT-Wazalendo.

error: Content is protected !!