Saturday , 9 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Msajili aipa siku saba ACT- Wazalendo ijieleze
Habari za Siasa

Msajili aipa siku saba ACT- Wazalendo ijieleze

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
Spread the love

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania, imekitaka Chama cha ACT-Wazalendo, kutoa maelezo ya ufafanuzi kuhusu mazungumzo yake na Ubalozi wa Uingereza nchini humo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Chama hicho kimetakiwa kuwasilisha maelezo hayo, ndani ya siku saba, kuanzia jana Ijumaa tarehe 12 Juni 2020 hadi saa 9:30 mchana wa tarehe 19 Juni 2020.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sisty Nyahozi, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa jana Ijumaa inaeleza kati ya tarehe 8 hadi 12 Juni 2020, Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, alifanya mazungumzo na Sarah Cooke, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar Es Salaam.

Taarifa ya Nyahozi inaeleza kuwa, kwa mujibu wa taarifa za mazungumzo hayo ambayo ofisi yake imezitoa katika vyombo vya habari, Zitto na balozi huyo walifanya kikao kwa ajili ya kupanga mikakati ya ushindi wa chama chake, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Kufuatia sakata hilo, Nyahozi amesema ACT-Wazalendo kinapaswa kujieleza kwa kuwa hatua yake hiyo imekwenda kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa, inayokataza mtu asiye Raia wa Tanzania kufanya vikao na viongozi wa vyama vya siasa.

“Hivyo kwa mujibu wa Kifungu cha 5B cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Msajili wa Vyama vya Siasa anawataka ACT-Wazalendo kuwasilisha maelezo yake kuhusu suala hilo, ili iweze kujua ukweli kuhusu taarifa hizo zilizoandikwa katika vyombo vya habari,” inaeleza taarifa ya Nyahozi na kuongeza:

“Maelezo yenu yawasilishwe Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa siyo zaidi ya tarehe 19 Juni 2020 saa tisa na nusu mchana.”

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira...

Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini...

error: Content is protected !!